Kagera River sekondari wapewa tahadhari dhidi ya wanaume
4 November 2024, 2:42 pm
Watoto wa kike wamekuwa katika hatari ya kushindwa kutimiza ndoto zao za kitaaluma kutokana na baadhi ya wanaume kuwafanyia ukatili wa kingono na wakati mwingine kuwasababishia mimba za utotoni
Na Ospicia Didace
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi UWT wilayani Karagwe mkoani Kagera Bi Georgina Mkapapa aliyeambatana na mwenyekiti wa bodi ya shule Bi Mastidia Rushambila wametumia sherehe za kuwakaribisha wa wanafunzi wa kidato cha tano iliyofanyika mwishoni mwa juma kuwataka wazazi na walezi kutimiza wajibu wa mahitaji ya watoto walioko shuleni hasa wanaosoma katika shule ya sekondari ya wasichana Kagera River iliyoko katika kata ya Kanoni wilayani Karagwe
Kwa pamoja viongozi hao wameonesha kukerwa na ongezeko la matukio ya ukatili dhidi ya watoto wa kike na kuwahimiza wazazi na walezi kubana matumizi ili watimize mahitaji ya watoto badala ya kuwaacha kukumbwa na vishawishi vya wanaume waharibifu
Mkuu wa shule ya sekondari ya wasichana Kagera River Bi Felister Francis (aliyesimama) akizingumza na wanafunzi. Picha na Ospicia Didace
Kwa upande wake mkuu wa shule ya sekondari ya wasichana Kagera river bi Felister Francis amesema kuwa hafla ya kuwakaribisha wanafunzi wa kidato cha tano mwaka huu ni kuzungumza nao kwa ajili ya kuwapa uzoefu wa mazingira na kuwahimiza kuzingatia lengo lao la kujiunga na shule hiyo ikiwa ni pamoja na kutumiza ndoto zao.
Baadhi ya wazazi wa wanafunzi wa kidato cha tano wakifuatilia maelezo ya mkuu wa shule. Picha na Ospicia Didace