Zenj FM

Ajali yaua watatu na kujeruhi 15 Tunguu

19 March 2025, 5:13 pm

Gari la mzigo yenye namba Z 578 GB aina ya Kenta iliyogongwa na gari yenye namba 273 NK ROUT Namba 339 ya Chuo Kikuu

Watu watatu wamefariki dunia na wengine kumi na tano (15) kujeruhiwa mara baada ya gari walokuwa wakisafiria kupata ajali huko Maeneo ya Tunguu Car wash.

Akithibitisha kutokea ajali hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Daniel Emanuel Shillah amesema gari yenye namba 273 NK ROUT Namba 339 ya Chuo Kikuu iliyokuwa ikiendeshwa na dereva Ahemid Faki Jecha mwenye umri wa miaka 32 mkaazi wa Daraja bovu gari yake iliacha njia na kuelekea upande wa pili wa barabara na kugonga gari ya mzigo yenye namba Z 578 GB aina ya Kenta iliyokuwa ikiendeshwa na Maulidi Mussa Makame mwenye umri wa miaka 46 mkaazi wa Magogoni.

Akitaja majina waliofariki dunia ni pamoja na dereva wa gari ya mizigo Maulid Mussa Makame, Haji Jecha Haji kondakta wa gari ya Chuo Kikuu, na watatu abiria ambae bado hajafahamika jina lake ambapo amesema sababu ya ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva wa gari ya route 339 chuo kikuu.

Sauti ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Daniel Emanuel Shillah.

Nae Daktari dhamana wa hospitali ya Wilaya Mwera Pongwe Dokta Mohd Mambi amekiri kupokea majeruhi 18 kati ya hao watatu wamepewa rufaa kwenda hospitali kuu ya Mnazi Mmoja na wawili wako katika chumba cha uangalizi wa daktari, na waliobaki wamepatiwa matibabu na kuruhusiwa kurudi nyumbani.

Sauti ya Dokta Mohd Mamb.

Mapema Mkuu wa Wilaya ya Kati Gallos Nyimbo amefika katika hospitali ya Wilaya mwera Pongwe kuwaona majeruhi wa ajali hiyo na kuwaombea kwa Mwenye enzi Mungu wapone kwa haraka na kuwataka ndugu na jamaa walioondokewa na watu wao kuwa na moyo wa subra katika kipindi hiki kigumu cha maombelezi huku akiwataka maderva kuachana na mwendo wa kasi ili kuepusha ajali.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Kati Gallos Nyimbo.

Nao mashuhuda wa ajali hiyo ametoa wito kwa madereva kufuata taratibu za barabarani ikiwemo ya kutoendesha mwendo mkubwa kwa kisingizo cha kukimbilia abira pamoja na kuwa makini wakati wote wakiwa barabarani hususani kipindi hiki cha mvua ili kuepusha ajali.

Sauti ya shuhuda.