Zenj FM

Kati ya baa 93, baa 33 zimefanikiwa kufunga vizuia sauti Zanzibar

5 December 2024, 5:40 pm

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na  Idara Maalum za SMZ  Masoud Ali Mohammed Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar.

Na Mary Julius.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na  Idara Maalum za SMZ  Masoud Ali Mohammed amesema Zanzibar kuna jumla ya maeneo yanayotoa  huduma ya Vileo (baa) 93 ambayo yamesajiliwa na kupewa leseni ya kufanya  biashara ya vileo kwa mwaka 2024.  

Waziri Masoud ameyasema hayo  katika kikao cha Baraza la Wawakilishi Chukwani, Zanzibar, wakati akijibu swali la mwakilishi Jimbo la Mwanakwerekwe Ameir Abdalla Ameir lenye sehemu 3 aaliye taka kujua (a)  Zanzibar kuna baa ngapi ambazo zimesajiliwa rasmi.

(b)  Je, ni vigezo gani na utaratibu upi hutumika kuzisajili baa hizo.

(c) Je, ni baa ngapi kati ya hizo zimetimiza sharti la vizuizi sauti na ngapi bado  hazijatimiza.

Waziri amesema usajili na utoaji wa leseni kwa biashara ya uuzaji wa vileo  hutolewa kwa mujibu wa Sheria ya Kudhibiti Vileo namba 9 ya mwaka 2020 .

Aidha amesema,maeneo yanayotoa huduma ya Vileo (baa) 33 kati ya maeneo 93 ndiyo yaliyotimiza sharti la kufunga vizuia sauti na maeneo 60 hayajatimiza sharti hili ambapo Serikali tayari imeshayafungia kupiga mziki.

Sauti ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na  Idara Maalum za SMZ  Masoud Ali Mohammed.