Zenj FM

Wazazi waaswa kuwapatia huduma za msingi watoto wenye ulemavu

22 November 2024, 7:25 pm

Mwakilishi  viti maalum Mwantatu  Mbaraka Khamisi akiwa na viongozi wa Umoja wa Watu wenye ulemavu Zanzibar pamoja na wazazi na watoto wenyeulemavu na wasio na ulemavu, katika viwanja vya Forodhani Zanzibar.

Na Mary Julius

Mwakilishi  viti maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM anayewakilisha kundi la  watu wenye ulemavu  Mwantatu  Mbaraka Khamisi amewataka wazazi kuwapatia huduma za msingi watoto wenye ulemavu kuwajenga kutokana na ulemavu wao ili nao waweze kujitegemea.

Akizungumza huko Forodhani katika tamasha la michezo kwa watoto wenye ulemavu lililoandaliwa na Umoja wa Watu Wenye Ulemavu Zanzibar Mwantatu amesema ni faraja kucheza na watoto wenye ulemavu ambao mara nyingi wamekuwa hawashiriki katika mambo ya kijamii.

Aidha amewataka   wazazi kutambua kuzaa watoto wenyeulemavu ni majaliwa ya Mungu lakini kuwa na ulemavu sio mwisho wa maisha na kwa kulitambua hilo serikali ya mapinduzi ya Zanzibar imejitoa ilikuona kila mtu anapata huduma za msingi.

Sauti ya Mwakilishi  viti maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM anaye wakilisha kundi la  watu wenye ulemavu  Mwantatu  Mbaraka Khamisi.

Akizungumzia Mradi wa  Huduma za Marekebisho kwa Watoto wenye Ulemavu CBR amewaomba wafadhili kusaidia umoja wa watu wenye ulemavu hasa katika program hiyo ili waweze kuwafikia watoto majumbani nakuona watoto wote wanapatiwa huduma na badae wawezekujitegemea.

Mwakilishi  viti maalum kupitia chama cha mapinduzi ccm anaye wakilisha kundi la  watu wenye ulemavu  Mwantatu  Mbaraka Khamisi.

Mkurugenzi wa Umoja wa Watu Wenyeulemavu Zanzibar Asia Abdulsalam Hussein amesema kuelekea siku ya watu wenye ulemavu duniani disember 3, umoja huo umeanda shughuli mbalimbali ikiwemo ya kuwakusanya watoto wasio na ulemavu kwa kuwajumuisha na watoto wenye ulemavu ili nao wajione kama watoto wengine pamoja na kuwahamasisha wazazi kuwatoa na kuwapatia watoto wenye ulemavu mahitaji yao ya masingi.

Sauti ya Mkurugenzi wa Umoja wa Watu Wenyeulemavu Zanzibar Asia Abdulsalam Hussein

Akizungumzia mradi wa Huduma za Marekebisho kwa watoto wenye ulemavu CBR Mkurugenzi Asia amewaomba wafanyabiashara na wafadhili kufadhili mradi huo ili kuweza kuwafikia watoto majumbani na kujua changamoto zao pamoja na kuwasogezea huduma za mazoezi.

Sauti ya Mkurugenzi wa Umoja wa Watu Wenyeulemavu Zanzibar Asia Abdulsalam Hussein

Kwa upande wao wazazi wa watoto wenye ulemavu wamewashukuru Umoja wa Watu Wenye ulemavu kwa kuwatoana kujumuika na  watoto wenzao ambapo wamepata faraja  ya kuona kuwa kuna watu wanawajali.

Aidha wazazi hao wameahidi kuwapatia watoto wao mahitaji muhimu kadri ya uwezo wao pamoja na kuwatoa nje ili wajumuike na watoto wenzao.

Sauti za wazazi wa watoto.

Lazziz Bakery ni wafadhili walio dhamini tamasha hilo kwa kutoa chakula kwa watoto wenye ulemavu wamesema wamefadhili tamasha hilo ili watoto hao wajisikie na kujiona wapo sawa na wengine.

Sauti ya mpishi Mkuu wa Lazziz Bakery Hussein Rashid.