Zenj FM

Cp. Hamad ahimiza kufanya kazi kwa kushirikiana

23 October 2024, 5:29 pm

Kamishna wa Polisi Zanzibar Cp. Hamad Khamis Hamad akizungumza wakati akifunga mafunzo ya Usalama wa Mazingira na Uchumi wa Bluu Zanzibar

Na Omar Hassan.

Kamishna wa Polisi Zanzibar Cp. Hamad Khamis Hamad amefunga mafunzo ya Usalama wa Mazingira na Uchumi wa Bluu na kuhimiza kufanya kazi kwa kushirikiana baina ya Vikosi vya Ulinzi na jamii kufikia malengo na Matarajio ya Serikali katika kuinua uchumi kupitia utalii na uwekezaji.

Huko Chuo cha Polisi Zanzibar Cp. Hamad akawahimiza Askari wa Jeshi la Polisi na Vikosi vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar walioshiriki mafunzo hayo ya wiki mbili kufanya kazi kwa uzalendo katika kuimarisha Amani ya nchi.

Sauti ya Kamishna wa Polisi Zanzibar Cp. Hamad Khamis Hamad.

Nae Kaimu Mkurugenzi wa Wizara ya Utalii Zanzibar Ashura Omar Ali amesema kupitia mafunzo hayo ya Usalama wa Mazingira na Uchumi wa bluu Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale ina matarajio ya kuhuimarika kwa fukwe na tamaduni.

Sauti ya Kaimu Mkurugenzi wa Wizara ya Utalii Zanzibar Ashura Omar Ali.

Kwa upande wake Mratibu wa Mafunzo hayo Dkt. Hassan Issa Ali kutoka Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar amesema kuna umuhumu wa kuthaminiwa na kutunzwa Mandhari nzuri ya Zanzibar kwani ameeleza kwa wananchi wengi wa Zanzibar hawafahamu thamani na uzuri wa Visiwa vya Zanzibar.

Sauti ya Mratibu wa Mafunzo hayo Dkt. Hassan Issa Ali.