Jeshi la Polisi Zanzibar lazindua kampeni maalum ya kutoa elimu ya udhalilishaji kwa wanafunzi
16 October 2024, 4:23 pm
Na Mulkhat Mrisho na Salhiya Hamad.
Katibu wa Baraza la Elimu na Mrajisi wa Elimu Zanzibar Faridi Ali Muhamad ameliomba Jeshi la Polisi kushughulikia kesi za udhalilishaji ili kuondoa vitendo hiyo katika jamii.
Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni ya tuwaambie kabla hawajaharibiwa uzinduzi ulio fanyika katika viwanja vya mao Zedong mkoa wa Mjini Magharib mesema kucheleweshwa kwa upelelezi wa kesi za udhalilishaji kunasababisha kuwakatisha tamaa wazazi katika kuziripoti kesi hizi katika vituo vya polisi,
Amesema wizara ya elimu imejiandaa kushirikiana na jeshi la polisi katika kuunga mkono kampeni hii ili kuwalinda wanafunzi na vitendo vya udhalilishaji.
Aidha Amewataka wazazi kuacha muhari katika kuripoti vitendo vya udhalilishaji hasa unao fanywa na ndugu wa karibu ili kuwalinda watoto na vitendo vinavyo fanywa na ndugu hao.
Nae Kamishina wa Polisi Zanzibar Cp Hamad Khamis Hamad amesema lengo la kampeni hiiyo nikuwapa uwezo wanafunzi wa kujitambua na kuelewa jinsi ya kujilinda dhidi ya hatari za unyanyasaji wa kijinsia pamoja na kuwaelimisha juu ya haki zao na kuwasaidia ni wapi wanaweza kupata masaada pindi wanapo pata matatizo
Aidha Cp Hamad amesema kampeni hii itasaidia wizara ya elimu katika kuendeleza elimu bora na salama kwa watoto kwani hakuna mwanafunzi anayeweza kupata elimu bora ikiwa anaishi kwa hofu ya kunyanyaswa au anatendewa vitendo vya udhalilishaji.
Akizungumza katika uzinduzi huo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharib SACP Richard Thadei Mchovu amesema matendo ya udhalilishaji wa kijinsia vinawaharibu watoto kwa kiwango kikubwa sana.
Kamanda Richard amesema Jeshi la Polisi limeona miongoni mwa njia zitakazowasaidia watoto kujikinga na vitendo hivi ni kufanya kampeni maalum ya kutoa elimu endelevu kwa watoto wetu ili wajiepushe na mazingira yatakayofanya wafanyiwe vitendo hivi vya udhalilishaji.
Kwa upande wa wanafunzi walio huzuria katika uzinduzi wa kampeni ya tuwaambie kabla hawajaharibiwa wamesema wamefurahi sana kuletewa hii kampeni ambayo itawasaidia katika kujikinga na vitendo vya udhalilishaji .
Aidha wamewaomba wazazi kuwalinda watoto wao na kuwafatilia mienendo yao ili waweze kuwalinda na vitendo vya udhalilishaji.