Waathirika wa mafuriko Kyela washikwa mkono na Babylon
17 April 2024, 14:43
Mkuu wa Wilaya ya Kyela Josephine Manase amemmwagia sifa mkurgenzi wa kiwanda cha mafuta ya kupikia cha Covenant Edible Oil oili Babylon Mwakyambile kwa kuwa wa kwanza kutoa misaada kwa wahanga wa mafuriko.
Na Emmanuel Jotham
Mkuu wa Wilaya ya Kyela Josephine Manase amemshukuru mkurugenzi wa kiwanda cha Covenant Edible Oil Babylon Mwakyambile kwa kuwa mtu wa kwanza kuitikia wito wa kuwachangia wananchi waliokumbwa na mafuriko sehemu mbalimbali hapa wilayani Kyela.
DC Manase amesema kuwa kutokana na wananchi wengi kukumbwa na mafuriko na vyakula vyao kusombwa na maji, kupitia kitengo cha maafa wilaya wameanzisha mpango wa kuwatafuta wadau wa maendeleo wilaya ya Kyela ambapo amesema Babylon amekuwa mtu wa kwanza kuitikia wito huo.
Katika hatua nyingine DC Manase ametumia nafasi hiyo kuwaomba wadau wengine kuwachangia wananchi waliokumbwa na mafuriko, ikiwa ni njia sahihi ya kuwafariji wananchi hao waliofikwa na majanga hayo.
Kwa upande wake mwakilishi wa mkurugenzi wa kiwanda cha Covenant Edible Oil Frank Mwakapala amekabidhi debe kumi za mahindi, ndoo za mafuta ya kupikia plastiki tano, ikiwa ni jitihada za kuwafariji wahanga wa mafuriko wilayani Kyela.
Frank amemaliza kwa kutoa wito kupitia kitengo cha maafa wilaya kutosita kurudi kwa Babylon tena pale patakapokuwa na uhitaji ili kuendelea kutoa faraja kwa wahanga wa mafuriko.