Kyela:Samia Mgeni rasmi maridhiano day Mbeya
3 February 2024, 16:31
Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania dokta Samia Suluhu Hasan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika siku ya mamaridhiano day itkayofanyika machi 3 2024 mkoani Mbeya.Na Masoud Maulid
Kuelekea siku ya maadhimisho ya Maridhiano day yatakayofanyika march 3.2024 kamati ya maridhiano na amani wilaya ya kyela imehamasisha uchangiaji damu kwa hiari na kupata mwitikio mkubwa kutoka makundi mbalimbali.
Akizungumza na mwandishi wa habari mwenyekiti wa kamati hiyo Seth Mwaisaka amesema kutokana na agizo la kamati ya maridhiano mkoa wa mbeya kuzitaka kamati za wilaya zinahamasisha wananchi kuchangia damu kwa hiari kuelekea maadhimisho hayo.
Amesema kamati ya wilaya imeanza zoezi hilo kwa kuhamasisha wanafunzi wa shule za sekondari ya ipinda na kafundo sekondari kuchangia kwa hiari ambapo mwitikio umekuwa mkubwa.
Mwaisaka ameongeza kuwa malengo ya kila kamati kutoka wilaya zote mkoa wa mbeya ni kuhakikisha ifikapo tarehe ya maadhimisho iwe tayari imekusanya damu uniti hamsini ambapo kwa mkoa mzima wa mbeya zipatikane uniti mia tatu,hivyo kutokana na uhitaji kuwa mkubwa ameiomba jamii kupitia makundi mbalimbali kujitokeza kuchangia ili kupata kiwango kingi cha damu salama.
Kwa upande wake mjumbe wa kamati hiyo Ibrahim Mwakaburi,amewapongeza Walimu na Wanafunzi wa shule hizo mbili kwa kujitokeza kuchangia kwa hiari ili kuwasaidia wahitaji,wakiwemo akina mama wanaopoteza damu nyingi wakati wa kujifungua,hivyo amewaasa wananchi makundi ya waendesha bodaboda,mashabiki wa simba na yanga pamoja na taasisi za kidini kuwa tayari kuchangia kwa hiari zoezi litakapofika kwenye maeneo yao
Nao wanafunzi wa shule ya kafundo sekondari na ipinda sekondari wamesema,wamejitolewa kutoa damu kwa hiari kutokana na kupata elimu kutoka kwa wataalamu juu ya umuhimu wa kuchangia damu na kuongeza kuwa,wamekuwa wakifanya zoezi hilo mara nyingi wanapohitajika na hakuna madhara yoyote wanayoyapata baada yakuchangia damu
Jumuia ya maridhiano na Amani imeanzishwa kitaifa mwaka 2016 mwezi march hivyo kila mwaka hufanyika amaadhisho ambapo kitaifa mwaka huu yatafanyika jijini mbeya na mgeni rasmi ni Rais wa Jamhuri ya muungano wa tanzania Dr Samia Suluhu Hasan