Kyela: Isaki waoga noti za Babylon Mwakyambile
26 January 2024, 01:53
Wanachama wa chama cha Mapinduzi hapa wilayani kyela wametakiwa kuungana ili kukamirisha ujenzi wa jingo la ofisi za kata Isaki hapa wilayani Kyela ili kuondoa kadhia ya kuwafuata viongozi wa chama nyumbani kwao.
Na James Mwakyembe
Mdau maendeleo na mwanachama wa chama cha Mapinduzi Ccm ambaye pia ni mkurugenzi wa kiwanda cha kuzarisha mafuta cha Convenant Edible Oil Ltd Kyela Cooking Oil Babylon Mwakyambile amekabidhi mifuko 25 ya saruji pamoja na fedha taslimu shilingi laki moja kuchangia ujenzi wa ofisi za kata Isaki hapa wilayani Kyela.
Saruji hiyo inayogharimu zaidi ya shilingi laki tano za kitanzania inatolewa na mdau huyo baada ya kuwepo kwa mkwamo wa ujenzi wa jengo hilo la ofisi kwa zaidi ya miaka kumi kutokana na kutokuwepo kwa fedha za kuendeleza ujenzi hali iliyolazimu uongozi wa kata kutafuta wadau ili kuwasaidia kukamilisha jengo hilo.
Akizungumza wakati wa hafra ya kukabidhi mifuko hiyo ishirini na mitano pamoja na fedha taslimu shilingi laki moja Mwakyambile amesema ameguswa na kuchangia ujenzi huo kutokana na umuhimu wa jengo hilo kwa viongozi wa chama na serikali katika kutekeleza majukumu yao ya kiofisi kama dira iliyooneshwa na mwenyekiti wa Ccm Taifa Samia Suluhu Hasani.
Babylon amewapongeza waasisi wa wazo lao la ujenzi na hatua waliyoifikia pamoja na kuwataka wanachama hao kushikamana katika kuhakikisha jengo hilo linakamilika kwa wakati pamoja na kuwaomba wadau wengine kujitokeza kuungana ili kuweka alama ya utambulisho miongoni mwao.
Kwa upande wa wanachama cha Mapinduzi Isaki wao wamemshukuru mdau huyo kwa msaada huo na kumuomba kuendelea kuwaunga mkono katika kazi hiyo ambayo yeye amekubali kushikamana nao hadi mwisho wa kukamilika kwa jengo hilo
Kadharika viongozi wa jumuiya ya vijana Ccm kupitia katibu wao wamemuomba Babylon Mwakyambile kuwaunga mkono katika suala la michezo ambapo jumuiya hiyo inatarajia kuanzisha ligi ya mpira wa miguu katika kata hiyo ikishirikisha timu nne lengo likiwa na kuwaweka vijana pamoja.
Kuhusu ombi hilo Mwakyambile amekubali ambapo ameahidi kutoa mpira mmoja pamoja na jezi kwa kila timu shiriki huku akiwataka viongozi hao kuendelea kuwakusanya vijana kwa kuwa mpira sasa ni ajira.
Huu ni muendelezo wa jitihada za mdau na mwananchama huyo wa Ccm hapa Kyela za kuhakikisha anaungana na wanachama wenzake wa chama cha mapinduzi wilaya ya Kyela katika kuhakikisha wanatatua changamoto ya ukosefu wa ofisi za kisasa katika maeneo mengi hapa wilayani Kyela pamoja na kuboresha ofisi hizo.