Kukaja Kununu wamwaga bima za afya Kyela
4 January 2024, 13:02
Katika kuhikikisha watoto wanakuwa na afya bora hapa nchini umoja wa kikundi cha Kukaja kununu kimetoa bima za afya na vifaa vya usafi vyenye thamani ya zaidi ya shilingi laki tano katika hospitali ya wilaya ya Kyela.
Na James Mwakyembe
Umoja wa kukaja kununu hapa wilayani Kyela wametoa vifaa vya usafi na kusafisha mazingira ya hospitali ya wilaya ya Kyela vyenye thamani ya zaidi ya shilingi laki tano za kitanzania.
Tukio hilo linafanyika ikiwa ni sehemu ya umoja huo kutekeleza majukumu yao ya kila siku ambayo wamejiwekea kwa kila mwaka ambapo mbali na kutoa vifaa hivyo pia wametoa bima za afya kwa watoto wapatao hamsini hapa wilayani Kyela.
Akizungumzia tukio hilo mwenyekiti wa umoja huo wa Kukaja Kununu Nelson Kibona amesema malengo mahususi ya kufanya jambo hilo ni kuunga mkono jitihada za serikali katika kuboresha huduma za sekta ya afya hapa nchini.
Akizungumza kwa niaba ya mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Kyela katibu ya hospitali hiyo Shazi Lunyambi amewashukuru umoja huo wa kukajaa kununu kwa jinsi walivyojitoa katika kuunga mkono jitihada za serikali katika kuboresha huduma za afya.
Wakizungumza kwa niaba ya watoto hamsini waliopatiwa bima za afya watoto fulan Tusajigwe Mwamkamba pamoja na Isaya Mwendapole wamewashukuru wanakikundi kwa miasaada hiyo kwani itawasaidia katika kupata mahitaji muhimu hasa ya kiafya kama ilivyokusudiwa.
Umoja wa kikundi cha kukaja kununu kilianzishwa kwa lengo kuu la kusaidia jamii ya wanakyela katika mambo mbalimbali ya kijamii ambapo katika mwaka 2023 kikundi hicho kimefika katika hospitali ya wilaya ya Kyela na kutoa vifaa vya usafi pamoja na kugawa bima za afya kwa watoto hamsini ili ziwasaidie katika matibabu.