Keifo FM

Mwalusangani awalilia wadau kukamilisha ujenzi zahanati ya Nkuyu

16 December 2023, 11:40

Picha ni jengo la Zahanati ya Nkuyu likiwa katika hatua ya boma baada ya nguvu za wananchi.Picha na James Mwakyembe

Wadau wa maendeleo wilayani Kyela wameombwa kusaidia ujenzi wa zahanati ya Nkuyu iliyokwama kumalizika kutokana na ufinyu wa bajeti.

Na James Mwakyembe

Baada ujenzi wa zahanati ya Nkuyu kukwama kumalizika kwa wakati uliopangwa diwani wa kata ya Nkuyu Hezron Mwalusangani amewaomba wadau mabimbali kujitokeza kusaidia kumalizia ujenzi huo muhimu kwa wananchi wa kata yake.

Hayo yamejiri baada ya Keifo fm kudhuru ndani ya kata hiyo kutaka kujua sababu za mkwamo huo ambapo Mwalusangani ameweza kubainisha kuwa tayari wananchi wamekamirisha jukumu lao la msingi ambalo ni ujenzi wa boma ambalo mpaka sasa limekwisha kukamirika.

Amesema hatua zilizobakia ni zile zinazohitaji uungwaji mkono kutoka serikalini lakini kutokana na ufinyu wa bajeti imekuwa kikwazo kukamirisha ujenzi huo kwa hatua za upauaji hivyo kuwaomba wanankuyu waishio nje ya wilaya ya kyela na wadau mbalimbali wa maendeleo kuwasaidia katika jambo hilo muhimu kwa afya za wanankuyu na taifa kwa ujumla.

Sauti ya diwani wa Nkuyu Hezron Mwalusangani ombi kwa wadau
Picha ya diwani wa kata ya nkuyu Hezron Mwalusangani

Pia Mwalusangani ameiomba serikali kuitazama Zahanati ya Nkuyu katika bajeti ijayo ya mwaka 2024 na 2025 ili kuwahakikishia wananchi wa Nkuyu afya iliyobora kwa kukamirisha ujenzi huo unaotarajiwa kuwa mkombozi kwa wakaazi wa vitongoji hivyo na vya jirani kama Serengeti na baadhi ya wakazi wa kaya ya Mwaya.

Sauti ya diwani wa Nkuyu Hezron Mwalusangani ombi kwa serikali halmashauri na mamlaka ya mji mdogo wa Kyela kuweka nguvu

Kwa upande wa mwenyekiti wa kitongoji cha Igombola kilichopo ndani ya kata hiyo Bambi Mwambungu amesema kwa ushirikano na viongozi wengine wameshirikiana kufikisha ujenzi huo katika hatua ya boma licha ya kadhia mbalimbali kuwepo wakati wa ujenzi huo.

Sauti ya Mwenyekiti wa kitongoji cha Igombola Bambi Mwambungu kuomba wadau pia

Amemaliza kwa kuishukuru serikali na vingozi mbalimbali wa wilaya ya Kyela wakiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Katule Kingamkono  kwa ushirikiano wanaouonesha kwa kila jambo na kuwatakia heri ya Krismas na Mwaka mpya wenye heri na Baraka kwao.