Mfungata:Tutaendelea kujenga lami zaidi Kyela
16 December 2023, 11:27
Serikali ya Tanzania chini ya Raisi Samia Suluhu Hasani imepanga kujenga barabara zinazogawa mitaa ndani ya Wilaya ya kyela katika bajeti ya 2023-2024.
Na Nsangatii Mwakipesile
Wakati serikali ikiendelea kutekeleza Miradi mbalimbali hapa nchini mhandisi wa TARURA Karim Mfungata ametoa shukrani kwa wananchi wilayani Kyela kwa ushirikiano wanaompa katika utekerezaji wa miundombinu iliyochini yake mijini na vijijini.
Hayo yamejiri mapema leo wakati akizungumza na Keifo Fm akiwa ofisi kwake ambapo Mfungata amesema tangu afike ndani ya wilaya ya Kyela hajawahi kukumbana na kadhia yoyote iliyopelekea kukwama kwa kazi zake tofauti na maeneo mengine.
kuhusu ujenzi wa barabara zinazoendelea kujengwa kwa kiwango cha lami hapa wilayani kyela amesema TARURA wanaendelea na ujenzi maeneo mbalimbali hasa hapa mjini ambapo amebainisha kuwa barabara zote zinaendelea kujengwa zitajengwa kwa kiwango cha lami.
Kuhusu mikakati iliyopo kwa mwaka ujao Mfungata amesema ni kuendeleza kuboresha matengenezo zaidi kama ujenzi wa matuta pamoja na kujenga barabara zingine kwa kiwango cha alami mjini na vijijini.
Aidha Mfungata amewataka wananchi kuitunza miuondombinu ya barabara zote zilizokwisha kujengwa na kumshukuru raisi wa jamahuri ya muungano wa Tanzania kwa kutoa fedha nyingi zinazoendelea kuwaletea tija wakaazi wa kyela.
Kukamilika kwa baadhi ya barabara kwa kiwango cha lami ndani ya wilaya ya Kyela kunatazamiwa kupunguza kadhia kubwa ya maji kujaa katika makazi ya watu kutokana na jiografia ya wilaya kukumbwa na mafuriko yanayotokana na mvua nyingi zinazopatikana katika majira ya mwaka.