Kyela:Nguvu ya wananchi yatumika kukarabati miundombinu ya barabara Ipyana B
9 December 2023, 17:29
Pichani Ni wananchi wa Kitongoji cha Ipyana B wakiwa katika zoezi la uchongaji wa barabara za mitaa za balozi mbili zilizoungana.Picha na Nsangatii Mwakipesile
Katika kuhakisha wanaunga mkono jitihada za serikali za kujiletea maendeleo miongoni mwao wananchi wa balozi mbili kitongoji cha Ipyana B wameungana na kuanza kuchonga barabara kwa nguvu zao wenyewe.
Na James Mwakyembe.
Wananchi wa kitongoji cha Ipyana B wameungana na serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuboresha miundombinu ya barabara baada ya kuamua kuanza kuchonga mifereji ili kupisha maji kuelekea katika kipindi cha mvua za masika.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi waliojitokeza kwenye zoezi hilo mwenyekiti wa kitongoji cha Ipyana B Betweli Betweli amesema baada ya kuwasilisha ombi la kuletewa makaravati kukwama kutokana na ufinyu wa bajeti wao wameamua kuungana na wananchi wa balozi mbili ili kuboresha barabara zao kupisha usumbufu wa maji nyakati za mvua za masika.
Kwa upande wa diwani wa kata ya Ipyana Gibonce Mwambije amewapongeza wananchi wa kitongoji hicho cha Ipyana B kwa uwamuzi huo akisema licha ya fedha kutokidhi uchongwaji wa barabara na makaravati wao wameungana kufanikisha jambo hilo hukuakisema umoja ni nguvu.
Kwa niaba ya balozi mbili zilizoshiriki kuanza kuboresha miundombinu ya barabara za kitongoji cha Ipyana B wao wamesema uamuzi huo umekuja kufuatia kuwepo kwa kadhia kubwa ya barabara hizo kupitika kwa shida au kutopitika kabisa nyakati za mvua za masika.
Ukumbukwe kuwa haya yanajiri ikiwa nchi yetu ya Tanzania inaadhimisha miaka sitini na mbili ya uhuru ambapo wananchi wa kitongoji cha Ipyana B wao wameamua kuungana na kutengeneza mifereji ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita chini ya rais Samia Suluhu Hasani.