Kayombo: Nilipanda mtini nyuki wakanishambulia
4 December 2023, 12:08
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jila la Rudigel Kayombo mkazi wa Makwale wilayani Kyela amevinjika uti wa mgongo baada ya kuanguka kutoka juu ya mti.
Na Masoud Maulid
Rudigel Lucas Kayombo mwenye umri wa miaka 61 mkazi wa kijiji cha Ibale kata ya Makwale wilaya ya Kyela anaomba msaada wa fedha kwa wasamaria wema kwa ajili ya kupata matibabu baada ya kuanguka kutoka juu ya mti wakati akifanya usafi wa shamba lake na kuvunjika mkono na uti wa mgogo.
Akizungumza na mwandishi wa habari Ludigel amesema tatizo hilo limetokea Disemba mwaka jana wakati akipogolea migomba iliyopo shambani kwake ambapo alipanda juu ya mti kuendelea na zoezi la usafi wa shamba ambapo juu ya mti huo alikuta nyuki ambao walimshambulia na kuanguka chini.
Baada ya kudondoka alivunjika mkono wa kushoto pamoja na uti wa mgongo ambapo alikimbizwa hospitali ya Wilaya ya Kyela kwa ajili ya matibabu,ambapo kutokana na hali kuwa mbaya alipewa Rufaa ya kwenda Hospitali ya Rufaa Mbeya kupatiwa matibabu huku tatizo kubwa mpaka sasa ni maumivu ya mgongo.
Kayombo ameeleza kuwa baada ya kushindwa kumudu gharama za matibabu alilazimika kuomba ruhusa kurudi nyumbani kwa ajili ya kutafuta fedha,lakini hadi sasa hajafanikiwa kupata fedha kwa ajili ya kurudi hospitali,hivyo amewaomba watanzania kumsaidia ili aondokane na mateso anayoyapata kwa sasa.
Kwa upande wa Mke wake Neema Ludigel Kayombo amesema toka Mume wake kupata matatizo hayo sasa ni muda wa miaka miwili na miezi mitatu,hali ya maisha imekuwa mbaya kutokana na Mume wake ndiye mtafutaji wa mahitaji ya familia kwa asilimia kubwa,hivyo anaiomba jamii kumsaidia fedha za matibabu ili kurudi kwenye hali yake ya kawaida.
Kiongozi wa kanisa lililopo kijiji cha Makwale kata ya matema amesema kanisa limetoa michango mingi kwa kushirikiana na jamii iliyomzunguka kwa lengo la kusaidia matibabu ya Rudigel Kayombo michango ambayo haijakidhi gharama za matibabu hivyo wanaiomba jamii ya watanzania kushirikiana pamoja ili kufanikisha matibabu.
Kwa yeyote mwenye kuguswa na tatizo hili na kuhitaji kumsaidia gharama za matibabu anaweza kuwasiliana nae au kutuma mchango wako kwenye namba 0783037439.