Jinsi teknolojia ya habari, inavyo weza kuinua uchumi kwenye vituo vya radio
12 September 2023, 10:58
Wandishi wa habari nyanda za juu kusini,wametakiwa kutumia Radio mtandao ili kufikisha habari kwenye jamii.na kuweza kuwafikia wadau kutoka sehemu mbalimbali nje na ndani ya Tanzania pamoja na kujipambambanua katika masoko ili kuinua uchumi kwenye vyombo vyao vya habari
Na Mwandishi wetu Emmanuel Jotham
Wandishi wa habari nyanda za juu kusini,wametakiwa kutumia Radio mtandao ili kufikisha habari kwenye jamii,na kuweza kuwafikia wadau kutoka sehemu mbalimbali nje na ndani ya Tanzania
Kauli hiyo imetolewa na mwezeshaji wa mafunzo kutoka Mtandao wa Radio jamii Tanzania(TADIO) Amua Rushita katika mafunzo yanayo endelea jijini mbeya yakihusisha Radio 9 wanachama kutoka mikao ya nyanda za Juu kisini.
Amesema endapo wandishi wa habari wataweza kutumia vizuri RAdio mtando kwenye Vituo vyao vya Radio wanaweza kuongeza uchumi kwenye Vituo kupitia matangazo mbalimbali watakayo yapata kupitia mtandao pamoja na kuziibua habari ambazo hazipewi kipa umbele na vituo vya habari vikubwa vya kitaifa.
Kwa upande wake Afisa miradi kutoka mtandao wa radio jamii tanzania TADIO SAUM BAKARI amesema lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha wandishi wa habari wanatumia teknolojia ili kuweza kupaza sauti ya habari zinazotokea kwenye jamii yao inayo wazunguka.
endapo wandishi wa habari wataweza kutumia vizuri RAdio mtando kwenye Vituo vyao vya Radio wanaweza kuongeza uchumi kwenye Vituo
Sauti ya Saum Bakari afisa miradi Tadio
Akizungumza kwa niaba ya washiriki wa mafunzo hayo Lusy Daud amesema kuwa mafunzo hayo yamekuwa na umuhimu mkubwa katika kuwaongezea uelewa wa kutumia mtandao kujitangaza na kutangaza vituo vyetu na katika kuhakikisha vituo vinajipambanua katika swala la masoko.
Sauti ya Lusy Dashud
Mtandao wa radio jamii Tanzania TADIO imekuwa ni kawaida kuwajengea uwezo wandishi wa habari Tanzania katika Nyanja mbalimbali ili kukuza ujuzi na mafanikio ya taarifa kwenye vituo vya Radiao .