Katule: Msikae kinyonge kanisa la Moravian ni kubwa
2 December 2023, 21:47
Wahitimu wa mafunzo ya uchungaji katika chuo cha biblia cha kanisa la kiinjiri Moraviani Tanzania hapa wilayani Kyela wametakiwa kumtegemea Mungu katika kazi yao mpya ya utumishi.
Na Nsangatii Mwakipesile
Mahafari ya kumi na tisa ya uchungaji ya chuo cha Biblia cha Kanisa la kiinjiri Moravian Tanzania yamefanyika leo katika majengo ya chuo hicho yaliyopo katika Kanisa la Moravian usharika wa Nkuyu na kuhudhuriwa na Mwenyekiti wa baraza la madiwani Kyela Katule Kingamkono.
Akizungumza mbele ya wahitimu hao saba Katule amewataka wachungaji hao kuwa kioo cha kanisa kwa kutenda kujitolea kuifanya kazi ya Mungu kwa Moyo na kumtanguliza yeye katika mambo yao yote.
Ameongeza kuwa kwa ukubwa wa kanisa la kiinjiri Moravian Tanzania inapaswa kuwa na majengo ya chuo chache lenyewe tofauti na hivi sasa ambapo wamekuwa wakitumia kanisa la Moravian usharika wa Nkuyu kama madarasa ya chuo hicho.
Awali akitoa neno mbele ya wahitimu na makutano walihudhuria maafari hiyo Askofu wa Kanisa la Kiinjiri Mpraviani Tanzania Joseph Mwambungu amewataka wachungaji hao kuwa askari walitayari kuipigana vita ya kiroho akitolea mfano safari ya wana wa Israeli kuifikia nchi yao ya ahadi ya kanani.
Akisoma risara mbele ya mgeni rasmi fulanifulani amesema licha ya kuhitimu leo chuo hicho kinakabiriwa na kadhia ya ukosefu wa majengo ambapo amesema mpaka sasa kama kanisa tayari wamepata tofari elfu nane na kuomba wadau kuwasaidia vifaa vingine vya ujenzi kama mchanga na saruji ili kufanikisha kuanza ujenzi huo.
Katika mahafari Katule Kingamkono amechangia shilingi laki tano fedha taslimu,mchanga tripu tatu na saruji mifuko mitano pamoja na kuahidi kuwa nao bega kwa bega pindi ujenzi huo utakapoanza.