Zahanati mpya ya kisasa yanukia Nduka
30 November 2023, 10:42
Baada ya kukosekana kwa huduma za afya kwa wananchi wa kijiji cha Nduka wilayani Kyela, serikali imepanga kujenga zahanati ya kisasa kijijini hapo.
Na James Mwakyembe
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kyela ambaye ni diwani wa kata ya Ikimba Katule Godfrey Kingamkono amempongeza diwani wa kata ya Ngana na watendaji wa kata ya Ngana kwa kuwarejesha wanafunzi watoro shuleni.
Pongezi hizo zimetolewa wakati wa ziara yake ya kakikazi ya kuhamasisha ujenzi wa Zahanati ya Nduka ambayo tangu kuanzishwa kwake hajawai kuwa na miondombinu ya afya.
Akizungumzia kuhusu ujenzi wa zanati Katule amewapongeza wananchi wa Nduka kwajitiada zao za kuhakikisha wanapata zanati hambayo inatarajiwa kuwa mkombozi na ustawi bora kwa wakazi wa Nduka hapa wilayani Kyela.
Kwa upande wa serikali Katule amesema tayari wamewasiliana na watalamu pamoja na madaktari ili kuangalia uwezekano wa kuanza ujenzi huo mara moja.
Kwa upande wa wananchi wamemshukuru mwenyekiti huyo na Diwani wao Aden Kajela kwa kusikia kilio chao na kuaidi kuwa wako tayari kushirikiana na serikali ili kuanza ujenzi huo na kukamilisha mara moja.
Nduka ni kitongoji kinacho patikana kijiji cha Ngana kata ya Ngana Hapa wilayani Kyela ambacho tangu uhuru kimendelea kukabiliwa na changamoto ya ukosefu wa mindombinu bora kama barabara, Elimu, Maji, na Afya.