

2 April 2025, 4:15 pm
Na Mary Julius.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kusini Unguja linamshikilia Mudriki Abdalla Msham, mwenye umri wa miaka 21 kwa tuhuma za kumbaka mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 17.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Daniel Shillah, amesema msichana huyo alikwenda kwenye viwanja vya sikukuu lakini alichelewa kurudi nyumbani, ambapo alipo rudi alikiri kuwa alikuwa nyumbani kwa mtuhumiwa.
Kamanda Shillah ameisisitiza jamii juu ya kuheshimu maadili na kuepuka vitendo vya udhalilishaji na kujihusisha kimapenzi na watoto walio chini ya miaka 18.