Zenj FM

Ujio wa wawekezaji toka Ubelgiji kuifungua Tanzania kiuchumi

29 November 2024, 5:03 pm

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji, Sharifa Ali Shariff. akifungua Kongamano la Biashara na Uwekezaji la Zanzibar na Ubelgiji lililofanyika katika hoteli ya Golden Tulip iliyopo uwanja wa ndege Zanzibar.

Na Mwanamiraji Abdallah.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji, Sharifa Ali Shariff amesema ujio wa wawekezaji kutoka Belgium ni Juhudi za Rais wa Zanzibar na Mwenyeketi Wa Baraza La Mapinduzi  Dk Hussein Ali Mwinyi na Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan za kuifungua Tanzania kiuchumi.

Waziri Sharifa ameyasema hayo wakati akifungua Kongamano la Biashara na Uwekezaji la Zanzibar na Ubelgiji lililofanyika katika hoteli ya Golden Tulip iliyopo uwanja wa ndege Zanzibar.

Kongamano hilo limewakutanisha Wafanyabiashara na Wawekezaji kutoka Zanzibar na Ubelgiji Kwa lengo la kujadiliana namna bora ya kuendelea kushirikiana ili kukuza biashara zaidi.

Aidha waziri amesema lengo la wawekezaji hao ni kuhakikisha kwamba wanatekeleza ipasavyo yale waliyoyaahidi na kuleta uwekezaji mkubwa katika nchi ya Tanzanzia hususani katika sekta ya uchumi wa buluu ,utalii na viwanda.

Sauti ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji, Sharifa Ali Shariff.

Naye, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Cosato Chumi (Mb.) Amewasihi kutembelea mikoa mingine ya Zanzibar kadri ratiba zao zitakavyoruhusu ili kuona maeneo mengine wanayoweza kuwekeza.

Kwa upande wake  mkurugenzi utawala na maendeleo rasilimali watu Zipa Vuwai Yahya Lada amesema lengo kubwa ni kuhakikisha wanakuza uchumi kupitia sekta za uwekezaji na mitaji binafsi kwani uchumi ni pato la taifa pamoja na ajira kwa vijana pia amesema “miradi kumi na moja 11 imeekezwa na beljium mingi yao ikiwa katika fursa za utalii na sekta za fedha miradi hii imeleta fursa kubwa sana za ajira na bado wanatarajia ongezeko kubwa la wawekezaji na kuleta pato la taifa “

Wafanyabiashara hao walitembelea pia eneo la ujenzi wa Bandari ya Mangapwani na wapo nchini Tanzania tangu tarehe 25 Novemba 2024 ambapo baada ya Kongamano hilo wanatarajia pia kuonana na viongozi mbalimbali wa Wafanyabiashara na Serikali kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaam na Zanzibar.