Zenj FM

UWT Zanzibar yawahakikishia wenye ulemavu fursa za mikopo

27 November 2024, 4:43 pm

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) na Makamo Mwenyekiti Wa Umoja Wa Wanawake Tazanzia Taifa UWT Zainab Shomari akikabidhi mtungi wa gesi kwa mmoja ya washiriki wa Kongamano la Watu Wenye Ulemavu.

Na Mary Julius

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) na Makamo Mwenyekiti Wa Umoja Wa Wanawake Tazanzia Taifa UWT Zainab Shomari amesema bado makundi la watu wenye ulemavu  halija faidika  na mikopo imayotolewa na serikali.

Makamo Mwenyekiti Zainab ameyasema hayo katika Kongamano la Watu Wenye Ulemavu lililoandaliwa na Umoja wa Watu Wenye Ulemavu Zanzibar UWZ  lililofanyika katika ukumbi wa Meli nne SACCOS Zanzibar, amesema umoja wa wanawake Tanzania UWT watapambana kuhakikisha mikopo ya halmashauri ya 4/4/2 inapatikana na kuwanufaisha watu wenye ulemavu kama ilivyo kusudiwa.

Aidha Makamo Mwenyekiti amesema Mikopo mingine imekuwa shida kwa watu wenyeulemavu kuifikia kutokana na vigezo na masharti yaliyowekwa.

Sauti ya Makamo Mwenyekiti Wa Umoja Wa Wanawake Tazanzia Taifa UWT Zainab Shomari.

Akizungumzia nishati safi na salama ya kupikia  Makamo Mwenyekiti Zanzibar amewapongeza waandaaji wa Kongamano hilo kwa kumuunga mkono kwa vitendo Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwapatiia majiko ya gesi watu wenye ulemavu ili nao kuondokana na kutumia nisharti isiyo salama kwa kupikia.

Sauti ya Makamo Mwenyekiti Wa Umoja Wa Wanawake Tazanzia Taifa UWT Zainab Shomari

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Umoja wa Watu Wenye ulemavu Zanzibar Asia Abdulsalam Hussein, amesema lengo la kongamano hilo ni kuwakutanisha kwa pamoja watu wenye ulemavu ili kujadili maswala yanayo wahusu ikiwemo maswala ya  kiuchumi, sheria  mbalimbali hasa iliyo pitishwa hivi karibuni.

Aidha Amewapongeza wadhamini wa kongamano hilo ikiwemo Mwakilishi Mwantatu  na Zaina kwa kuweza kutendea haki nafasi walizo pewa katika kuwawakilisha watu wenye ulemavu.

Sauti ya Mkurugenzi wa Umoja wa Watu Wenye ulemavu Zanzibar Asia Abdulsalam Hussein,

Kwa upande wake Mwakilishi Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM anayewakilisha kundi la watu wenye ulemavu Mwantatu Mbaraka Khamisi amesema lengo la kukutana hapo ni kutambua juhudi kubwa zilizo fanya na viongozi wakuu katika kuhakikisha watu wenye ulemavu wanapata mahitaji yao bila vikwazo pamoja nakuweka miundo mbinu wezeshi katika sekta mbalimbali.

Sauti ya Mwakilishi Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM anayewakilisha kundi la watu wenye ulemavu Mwantatu Mbaraka Khamisi

Nao washiriki wa kongamano hilo kutoka unguja na pemba wamesema kongamano hilo limeweza kuwajengea uwelewa wa mambo mbalimbali ikiwemo kuijua sheria ya watu wenye ulemavu na wajibu wao katika kuhakikisha wanazipigania haki zao za masingi.

Sauri ya washiriki

Mada tatu zilizo wakilishwa  katika Kongamano hilo kiwemo namna gani serikali imeangalia swala la uwezeshaji kiuchumi kwa watu wenye ulemavu na kwa jinsi gani  serikali imeweka miundo mbinu wezeshi ktika huduma muhimu kama vile afya elimu , mawasiliano na huduma nyingine muhimu nza kibinadamu na ya tatu  mkazo gani umewekwa kwenye sheria na sera zinazo walinda na kuwapa haki na fursa sawa watu wenye ulemavu.

Kongamano hilo ni muendelezo washamrashamra za  kuelekea siku ya watu wenye ulemavu December 3 ambapo kwa Zanzibar ikilele chake kitafanyika kisiwani pemba ikiwa na kauli mbiu ya ”kukuza uongozi wa watu wenye ulemavu kwa mustabakali  jumuishi na endelevu”