Zenj FM

Baraza la Mji Kati laahidi kumaliza miradi ya Madiwani kabla ya uchaguzi

25 November 2024, 5:28 pm

Kaimu Katibu Baraza la Mji Kati ambae pia ni Mkuu wa Idara ya Rasilimali Watu Mipango na Utawala Rehema Khamis Hassan pichani akiwa tayari kujibu Hoja za Wajumbe wa kikao cha Baraza la Madiwani kinachofanyika Kila robo Tatu ya Mwaka chenye lengo la kujadili mambo mbali mbali yahusuyo Utekelezaji wa shughuli za Baraza Hilo.

Wilaya ya Kati.

Kaimu Katibu Baraza la Madiwani Ofisi ya Baraza la Mji Kati ambae pia ni Mkuu wa Idara ya Rasilimali Watu Mipango na Utawala  Rehema Khamis Hassan, amesema miradi ya madiwani wilaya ya kati  inatarajiwa  kukamilika kabla ya kufikia kipindi cha uchaguzi ili kuwaweka wananchi   katika maeneo salama.

Rehema ameyasema hayo kwaniaba ya Mkurugenzi wa Baraza la Mji Kati Salum Mohamed Abubakar , wakati  wa kikao kilicho lenga kuangazaia Muelekeo wa Baraza la Mji Kati kwa Miezi Mitatu iliyopita Julai – Septemba na Miezi Mitatu ijayo kufuatia Kikao cha robo tatu ya pili Oktoba- Disemba kwa Mwaka wa fedha 2024-2025. amesema, miongoni mwa yaliyojadiliwa ni pamoja na ukusanyaji wa Mapato, Usafi wa Mazingira pamoja na Utekelezaji wa Miradi ya Madiwani.

Aidha amewataka wananchi kufika ofisini kwa ajili ya kulipa na kupata ushauri mbalimbali wa kibiashara  na kuepuka kuwaamini baadhi ya wafanyakazi.

Amesema Makadirio kwa Robo Tatu ya kwanza Juai- Septemba ni Shilingi milioni mia tatu thalasini na Tatu laki mbili na arobaini na nane elfu 333,248,000/=, ambapo wamefanikiwa kukusanya shilingi milioni miamoja thamanini na Tatu elfu sabiini na tisa mia Moja kumi na Tano elfu 183,079,115/=, sawa na asilimia 55% sambamba na Makadirio ya makusanyo ya taka Tani mia nane 800 na kufanikiwa kukusanya jumla ya Tani miasita ishirini na Tatu nukta saba 623.7 kwa upande wa Hoteli na Tani miamoja hamsini na nne nukta hamsini na nne 154.54 kwaupande wa taka za madukani.

Aidha  Makadirio kwa Robo Tatu ya pili Oktoba- Disemba ni kukusanya fedha zisizopungua shilingi milioni mia nne na sita laki nne tisiini na tisa mia sita na hamsini 406,499,650/=, ambapo jumla ya Tani 820 za taka kutoka katika Maduka na Hoteli za Wilaya ya Kati pia zinatarajiwa kukusanya kwa Maendeleo ya Taasisi na Wananchi kwa ujumla.

Sauti ya Kaimu Katibu Baraza la Madiwani Ofisi ya Baraza la Mji Kati ambae pia ni Mkuu wa Idara ya Rasilimali Watu Mipango na Utawala  Rehema Khamis Hassan.

Nae Mwenyekiti wa Baraza la Mji Kati ambae pia ni Diwani wa kuteuliwa  Said Hassan Shaabani amesema miongoni mwa Muelekeo wa Baraza la Mji Kati ni kuthibitisha Mpango Mkakati utakao onyesha muongozo wa Dira kwa Watendaji wa Ofisi hiyo katika majukumu yao ya Kila siku, pia amewataka Wananchi kuendelea kuamini kazi zinazofanywa na Watendaji wa Baraza la Mji Kati pamoja na kuziunga mkono jitihada za Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi juu ya kutekeleza Miradi ya Maendeleo katika kipindi cha miaka minne ya Uongozi wake.

Sauti ya Mwenyekiti wa Baraza la Mji Kati ambae pia ni Diwani wa kuteuliwa  Said Hassan Shaabani.