Zenj FM

Mkutano wa jinsia ni muhimu kwa Tanzania – DCP Chillery

18 November 2024, 6:00 pm

Mkuu wa Utawala na Rasilimali watu wa Jeshi la Polisi Kamisheni ya Zanzibar, Naibu Kamishna wa Polisi Dcp. Simon Thomas Chillery akifungua Mkutano wa siku tatu unaowahusisha Askari Polisi na wadau wa Amani wa Nchi za Afrika Mashariki kuhusu usawa wa kijinsia katika vyombo vya Ulinzi na Usalama.

Na Omar Hassan

Mkuu wa Utawala na Rasilimali watu wa Jeshi la Polisi Kamisheni ya Zanzibar, Naibu Kamishna wa Polisi Dcp. Simon Thomas Chillery amefungua Mkutano wa siku tatu unaowahusisha Askari Polisi na wadau wa Amani wa Nchi za Afrika Mashariki kuhusu usawa wa kijinsia katika vyombo vya Ulinzi na Usalama na na namna ya kushughulika na makosa ya kijinsia.

Mara baada ya Kufungua Mkutano huo Kwaniaba ya Kamishna wa Polisi Zanzibar huko Hoteli ya Madinat Al Bahri, Mbweni Zanzibar Naibu Kamishna Chillery amesema mkutano huo ni muhimu kwa Tanzania na Jeshi la Polisi katika kuzuwia uhalifu wa kisasa dhidi ya wanawake na watoto.

Sauti ya Mkuu wa Utawala na Rasilimali watu wa Jeshi la Polisi Kamisheni ya Zanzibar, Naibu Kamishna wa Polisi Dcp. Simon Thomas Chillery.

Nae Mtaalam wa sera na usalama wa wanawake kutoka Shilika la UN Women Idil Absiye ameeleza kuwa Shirika la UN Women pamoja na Shilika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na Uhalifu wa Dawa za kulevya, wamefadhili Mkutano huo ili kuwainua wanawake, kukuza usawa wa kijinsia na kuzuwia ukandamizaji dhidi ya wanawake na watoto.

Sauti ya Mtaalam wa sera na usalama wa wanawake kutoka Shilika la UN Women Idil Absiye.

Kwa upande wake Mkufunzi Mkuu wa Chuo cha Polisi Zanzibar, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Ssp. Pili Fobbe amesema Kitabu kinachohusu Jinsia kinachojadiliwa katika mkutano huo kitakuwa kinaendana na wakati katika kushughulika na uhalifu wa kisasa.

Sauti ya Mkufunzi Mkuu wa Chuo cha Polisi Zanzibar, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Ssp. Pili Fobbe.