Wananchi Micheweni watakiwa kushirikiana na Polisi Jamii
7 August 2023, 11:13 am
Kamishina Msaidizi wa polisi Dkt Emmanuel amesema bado kuna mwamko mdogo kwa wananchi wa micheweni katika kushirikiana na polisi jamii.
Na Omary Hassan.
Mkuu wa Polisi jamii Zanzibar, Kamishna Msaidizi wa Polisi Dkt. Egyne Emmanuel awewataka wananchi kuzitumia kamati za Ulinzi na usalama za Shehia kuwasilisha kero za uhalifu zilizopo katika mitaa yao ili zitafutiwe ufumbuzi kupitia kamati hizo.
Akizungumza na wananchi katika Kijiji cha Kiungoni Wilaya ya Wete na Kijiji cha Tumbe wilaya ya Micheweni amesema bado mwamko ni mdogo kwa wananchi kushirimkiana na kamati za ulinzi na usalama katika kubaini, kuzuwia na kutatua changamoto za uhalifu.
Kwa upande wao wananchi wa vijiji hivyo wameliomba Jeshi la Polisi kujipanga katika kusaidia nyenzo za kufanyia kazi kwa vikundi vya ulinzi shirikishi ili kuwe na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya kusimamia ulinzi na usalama wa wananchi katika Shehia.