Jamii, polisi kushirikiana kupambana na ongezeko la uhalifu Zanzibar
1 August 2024, 5:07 pm
Na Omar Hassan
DCP Zubeir Chembera amesema idadi ya baadhi ya makosa imepungua ikiwemo makossa ya kulawiti ambapo kuna upungufu wa makosa 24 sawa na asilimia 15.6.
Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Naibu Kamishna wa Polisi Zubeir Chembera ameitaka jamii kushirikiana na Jeshi la Polisi kupunguza uhalifu wa makosa mbalimbali yakiwemo ya Mauwaji, udhalilishaji na wizi ambayo yamekuwa yakiongezeka.
Akitoa Tathmini ya hali ya Uhalifu kamisheni ya Polisi Zanzibar kwa kipindi cha Januari hadi Juni 2024 huko Makao Makuu ya Polisi Zanzibar Chembera amesema Jumla ya Makosa makubwa 1,652 ya Jinai yameripotiwa ikilinganishwa na makosa 1,459 yaliyoripotiwa kipindi kama hicho mwaka 2023 kukiwa na ongezeko la makosa 193 sawa na asilimia 13.2.
Kwa upande wao Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja, Kamishna Msidizi Mwandamizi wa Polisi SACP. Daniel Emanuel Shillah na Mkuu wa Polisi Jamii Zanzibar, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Jonas Mahanga wamesema kufuatia tathmini hiyo wamepanga mikakati ya kufanya kazi kwa bidi, kongeza ushirikano na jamii pamoja na kutoa elimu kwa jamii juu ya kubaini na kuzuwia uhalifu.