Mufindi FM
Mufindi FM
2 November 2026, 2:09 pm

Mbunge wa Mufindi Kaskazini, Mheshimiwa Exaud Kigahe, amezindua Zahanati ya Kijiji cha Ihefu na kukabidhi vitanda viwili vya wagonjwa, huku akiwataka wananchi kuitunza miundombinu hiyo ili iendelee kutoa huduma bora za afya.
Na Jumanne Bulali.
Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kaskazini, Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa, Mheshimiwa Exaud Kigahe, amewataka wananchi kushirikiana katika kulinda na kutunza miundombinu ya afya ili iweze kudumu na kuendelea kutoa huduma bora kwa jamii.
Ametoa wito huo wakati wa uzinduzi wa Zahanati ya Kijiji cha Ihefu, Kata ya Mdabulo, ambapo pia amekabidhi vitanda viwili vya wagonjwa kwa lengo la kuboresha mazingira ya utoaji wa huduma za afya.

Awali, Diwani wa Kata ya Mdabulo, Mheshimiwa Marco Shayo, amesema kukamilika kwa zahanati hiyo kutawarahisishia wakazi wa Ihefu kupata huduma za afya karibu na makazi yao.
Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Mufindi, Dkt. Fredrick Jackoracha, amewahimiza wananchi kujiunga na bima ya afya ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za matibabu.
Ujenzi wa Zahanati hiyo ya Kijiji cha Ihefu umegharimu zaidi ya Shilingi Milioni 50.