Mufindi FM

DC Mufindi aandaa futari

9 April 2024, 10:33

Wananchi na waumini mbalimbali wa dini ya kiislamu wakishiriki futar iliyoandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Dkt. Linda Salekwa kwenye ukumbi wa Bomani. Picha na Marko Msafili.

Na Marko Msafili- Mufindi

Wakati waumini wa dini ya Kiislamu kote ulimwenguni wakiendelea na mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, waumini wa dini ya Kiislamu wilayani Mufindi wameshiriki futar iliyoandaliwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Dkt. Linda Salekwa.

Hafla hiyo imefanyika leo Jumatatu 08 April, 2024 katika ukumbi wa Bomani Mafinga ambayo imeongozwa kwa dua na Sheikh wa Wilaya ya Mufindi Sheikh Abubakari Ngwada.
Mara baada ya dua hizo, Mkuu wa Wilaya Hiyo Dkt. Linda Salekwa amewashukuru waumini wa dini hiyo kwa kuitikia wito na kuwataka waendelee kuliombea taifa sambamba na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Sambamba na hilo, Dkt. Salekwa amewataka Waumini hao waendelea kulinda amani ya nchi yetu, huku wakiendelea kuchapa kazi kwa adhima ya kutimiza wajibu wao kwa jamii.

Naye Sheikh wa Wilaya hiyo, Sheikh Abubakar Ngwada kwa niaba ya waumini wa wilaya hiyo wamemshukuru Dkt. Salekwa na serikali kwa kuandaa hafla hiyo na kwamba wanatamani zoezi hilo liwe endelevu.