Mufindi FM

Mitungi ya gesi inayotolewa inaambatana na utoaji elimu?

6 October 2023, 10:55

Mbunge wa Mufindi Kaskazini mh.Exaud Kigahe akipokea mitungi ya gesi kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Oryx gas, Benoit Araman, August 2023.

Mitungi ya gesi ambayo inatolewa na wabunge inalenga kupunguza athari za mabadiliko ya tabia ya nchi lakini inahitajika elimu ili kufikia lengo.

Na Marko Msafili/Mufindi

Kufuatia uwepo wa jitihada zinazofanywa na serikali katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi ikiwemo kugawa mitungi ya gesi, wananchi walionufaika na nishati ya gesi wameombwa kuendelea kuwa walimu kuhusu elimu sahihi ya matumizi ya mitungi hiyo ili kuepukana na visa vitokanavyo na nishati hizo.

Wito huo umetolewa na Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kaskazini Rajabu Mpinge wakati akizungumza na Mufindi Fm Radio 107.3 ambapo ameaarifu kuwa, mara baada ya kugawa mitungi ya gesi hakuna visa vyoyote vilivyoripotiwa vitokanavyo na Nishati ya gesi.

Sauti ya Rajabu Mpinge

Aidha Ndg. Rajabu amewasihi, wananchi kuendelea kushirikiana katika suala la mabadiliko ya tabia ya nchi kwa kuhakikisha vyanzo mbalimbali vinalindwa ili kuwezesha jitihada za kuhama kutoka matumizi ya nishati zisizo salama na kutumia nishati jadidifu.

Sauti ya Rajabu Mpinge

Ikumbukwe kuwa, Mhe. Exaud Kigahe, alikabidhi mitungi ya gesi 500 kwa wanawake wa jimbo hilo yenye thamani ya Sh milioni 50 zilizotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan, ambapo amesema amejipanga vizuri kumuunga mkono Rais Dkt. Samia katika kutunza mazingira na kuondokana na uharibifu.