Mufindi FM

Jukwaa la Wadau wa Parachichi

16 April 2024, 10:17

Wadau wa zao la parachichi wilayani Mufindi wakijadili kuhusu utatuzi wa changamoto zinazowakabili katika ukumbi wa MET mjini Mafinga.picha na Jackson Machowa-Mufindi

Na Jackson Machowa-Mufindi

Wakulima wa zao la parachichi wilayani Mufindi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali katika mnyororo wa thamani ya zao hilo wameungana na kuunda jukwaa la pamoja la zao hilo ili kupaza sauti itakayosaidia kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali na kuwezesha kukua kwa kilimo cha zao hilo.

Jukwaa hilo lililopewa jina la Jukwaa la Wadau wa Parachichi wilaya ya Mufindi limeundwa hii leo na wadau hao waliokusanyika katika ukumbi wa MET uliopo katika halmashauri ya mji wa mafinga na kuhudhuriwa na wanachama zaidi ya 50 kutoka katika maeneo mbalimbali wilayani humo.

Akizungumza kwa mara ya kwanza baada ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa jukwaa hilo Bwana Alban Lutambi amesema jukwaa hilo litasaidia kuwatangaza wakulima wa parachichi na hivyo kurahisisha upatikanaji wa soko la uhakika na lenye tija kwa wakulima.

Sauti ya Alban Lutambi

Kwa upande wake Afisa vijana na wanawake kutoka Feed the Future Tanzania kupitia mradi wa Kilimo Tija unaofadhiliwa na shirika la USAID, Bi Emelda Nguma amesema wameamua kuunga mkono jitihada za kuanzishwa kwa majukwaa hayo ili kukuza sekta ya kilimo na wakulima wake.

Sauti, ya Bi Emelda Nguma

Jukwaa hilo ambalo linatarajiwa kutambulishwa na kuzinduliwa rasmi mwishoni mwa mwezi mei mwaka huu, kwa sasa linasimamiwa na viongozi wa tano waliochaguliwa na wajumbe waliohudhuria mkutano huo ambao ni Alban Lutambi (Mwenyekiti), Emmanuel Kisinda (Katibu), Zainabu Mahenge (Katibu msaidizi), Awariyo Nnko (Muhasibu) Pamoja na wakuu wa divisheni za kilimo