Mufindi FM

RC Serukamba: Kijiji kwa kijiji

12 March 2024, 08:25

Mkuu wa mkoa wa Iringa Peter Serukamba akihutubia wakati wa makabidhiano ya ofisi. Picha na Moses Mbwambo.

Na Marko Msafili/Iringa
Marchi 10, 2024 yamefanyika Makabidhiano ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kati ya Mkuu wa sasa wa Mkoa huo Mhe. Pater Serukamba na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Halima Dendego ambaye amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoani Singida.
Akitoa salamu kwa Watumishi waliohudhuria Makabidhiano hayo yaliyofanyika katika Ukumbi mpya wa Ofisi ya Mkuu huo, Mhe, Serukamba amewataka Viongozi mbalimbali wa Mkoa huo kutenda haki kwa wananchi na kusema kuwa dhamira yake ni kutembelea kijiji kimoja badala ya kingine kwani haamini katika maneno ya kuambiwa.

Sauti ya Peter Serukamba

Aidha Mhe. Serukamba amesema, kabla ya kuanza shughuli mbalimbali atakutana na Viongozi wa Kilima wa Mkoa huo ili wampe Baraka katika utendaji kazi wake, huku akisema palipo na wazee hakuna jambo linaharibika.
Akizungumza Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Iringa Ndg. Hassan Makoba kwa niaba ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Kufanya mabadiliko madogo ikiwa ni katika utekelezaji wa ilani ya chama hicho.

Sauti ya Hassan Makoba

Aidha Nae Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa Mhe. Ibrahim Ngwada amempongeza Mhe. Halima Dendego kwa ushirikiano aliouonesha katika kipindi chote cha uongozi akiwa Mkuu Mkoa huo na kumsihi aendeleo na ubunifu aliounesha kwenye masuala mbalimbali.

Sauti ya Ibrahim Ngwada