Mufindi FM

Ziara ya Mbunge Mufindi Kaskazini Kata ya Kibengu

14 September 2023, 09:50

Mbunge wa Mufindi Kaskazini Mh. Exaud Kigahe (wa kwanza kushoto pichani) akiwa ziarani katika kata ya Kibengu wilayani Mufindi Jana. Picha na Kelvin Mickdady

Na Kelvin Mickdady-Mufindi

Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kaskazini ambaye pia ni Naibu waziri wa Viwanda na Biashara Mh. Exaud Kigahe ameahidi kuendelea kutekeleza miradi ya miundombinu iliyopo Jimboni kwake ili kuboresha huduma za kijamii.

Mh.Kigahe ameyasema hayo hii Leo wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Igeleke kata ya Kibengu kuwa ataendelea kusimamia miradi ya Maendeleo ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za kijamii ikiwemo Miundombinu ya Barabara kujengwa kwa kiwango cha rami.

Sauti ya Mh.Kigahe

Sambamba na hayo Mh.Kigahe amesema serikali inafanyia kazi suala la pembejeo kupatikana katika ujazo tofautitofouti ambapo pia amewasihi Vijana na Wafanyabiashara kuchangamkia fursa ya uwakala wa usambazaji wa pembejeo hizo.

Sauti ya Mbunge Mufindi Kaskazini

Awali wakizungumza wananchi wa Kijiji cha Kibengu na Kijiji cha Igeleke wamemuomba Mbunge Mhe. Kigahe kuwa wana matumaini naye huku wakimtaka kutatua kero zao.