Mufindi FM

Wilaya tatu mkoani Iringa zapewa elimu matumizi takwimu za sensa 2022

12 October 2023, 21:53

Mbunge wa jimbo la Mafinga Cosato Chumi na mratibu wa mafunzo ya matumizi ya matokeo ya sensa yaliyofanyika Mafinga mjini. Picha na Shalom Robert

Na Bestina Nyangaro-Mafinga

Halmashauri za Mufindi, Mafinga mji na Kilolo zimepatiwa mafunzo ya matumizi ya takwimu za matokeo ya sensa ya Sita iliyofanyika mwezi Agosti mwaka 2022.

Mafunzo hayo yametolewa hii leo katika ukumbi wa CCM Halmashauri ya mji Mafinga, yakilenga kutoa elimu ya namna ya utumiaji wa takwimu za matokeo ya sensa ya watu na makazi katika mipango jumuishi kwa maendeleo endelevu.

Kwenye mafunzo hayo yaliyoratibiwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwa kushirikiana na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Mafinga mjini,na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali ngazi ya mkoa kata hadi vijiji, yakijumuisha matumizi ya takwimu za idadi ya watu na takwimu za kijiografia.

Mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa mkoa wa Iringa Mh. Halima Dendego amesema ni wakati mwafaka wa kuhakikisha maendeleo yanapatikana bila upendeleo na kuelimisha wananchi waliyopo ngazi ya chini kutumia takwimu hizo.

Sauti Halima Dendego

Akitoa maelezo kwa niaba ya Mtakwimu mkuu wa serikali Dkt. Albina Chiwa, Meneja wa Takwimu mkoa wa Iringa Peter amesema zoezi hilo ni hatua ya tatu ambapo ilitanguliwa na uhamasishaji wa wananchi kushiriki kuhesabiwa kisha kufuatia na zoezi la sensa.

Sauti ya Peter Millinga

Nae mbunge wa Mafinga mjini Mh. Cosato David chumi baada ya mafunzo amesema yatasaidia kuwepusha mivutano katika mgawanyo wa mipango ya maendeleo katika maeneo Yao, huku miongoni mwa waliyohudhulia mafunzo hayo diwani wa kata ya Malangali ameeleza kushangazwa na takwimu za wazee kwenye kata yake.

Sauti ya Cosato Chumi
Sauti ya diwani Shakila

Tanzania imekuwa miongoni mwa nchi vinara ambazo zimefanikiwa kufanya sensa kila baada ya miaka 10 kati ya nchi 54 barani Afrika.