Mufindi FM

Malinyi kunufaika na klinik tembezi

10 October 2023, 09:04

Baadhi ya wakazi wilayani Malinyi wakishuhudia uzinduzi wa klinik tembezezi katika viwanja vya hospitali ya wilaya. Picha na Jackson Machoa

Na Jackson Machoa/Morogoro

Mkuu wa wilaya ya Malinyi mkoani Morogoro Mh. Sebastian Waryuba amezindua mradi wa klinik tembezi wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 210 uliofadhiliwa na nchi ya Uswiz kupitia shirika lisilo la kiserikali la Solider Med ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi wilayani humo.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mradi huo iliyofanyika katika viwanja vya hospitali ya wilaya, Mh. Waryuba ameipongeza nchi ya Uswiz kupitia shirika la Solider Med kwa ufadhili wa mradi huo na kuwataka watumishi wa afya kuutumia vyema mradi huo ili malengo yaliyokusudiwa yaweze kufikiwa.

Sauti ya DC Waryuba

Kwa upande wake Mkurugenzi mkazi wa shirika hilo Bwana Benatus Sambili amesema shirika la Solider Med lipo kwa muda mrefu nchini katika mkoa wa Morogoro na kwa muda wote huo limekuwa likishirikiana na serikali katika utoaji wa huduma bora za kiafya kwa wananchi.

Sauti ya Benatus Sambili

Katika hatua nyingine Bwana Sambili amesema nembo za shirika zilizopo nje ya gari ya ckinik hiyo hazihusiani na huduma zitakazotolewa kwani tayari mradi huo umeshakabidhiwa kwa serikali ya wilaya hivyo huduma zote zitakazotolewa kwenye clinik hiyo zitakuwa chini ya taratibu za kawaida za serikali na sio shirika.

Nae Meneja wa mradi huo Bi Frida Akyoo wakati akisoma risala ya mradi, amesema mradi huo unalenga kutoa huduma mbalimbali za kiafya katika kata zote kumi za wilaya hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia october 2023 hadi october 2025.

Sauti ya Bi. Frida

Hii ni kwa mara ya kwanza wananchi wa halmashauri ya wilaya ya malinyi hasa waishio katika maeneo yasiyofikika kirahisi watakuwa na uhakika wa kupata huduma za afya kutokana na uwepo wa mradi huo ambao utawafikia mpaka huko huko waliko.