Mufindi FM

Wananchi 350 waanza kutumia nishati safi ya kupikia

17 April 2024, 19:40

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mufindi George Kavenuke akikabidhi mtungi wa gesi, katikati ni mbunge wa Jimbo la Mafinga na wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa teknolojia ya nishati jadidifu na mbadala Advera Mwijage. Picha na Bestina Nyangaro

Na Bestina Nyangaro
Ofisi ya mbunge Jimbo la Mafinga Mjini kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati, imegawa mitungi 350 ya gesi ambayo imeambatana na elimu (Mafunzo) ya nishati safi ya kupikia kwa lengo la kuwezesha upatikanaji wa nishati hiyo.

Zoezi hilo limefanyika leo April 17, 2024 kama anavyoeleza mbunge wa Jimbo la Mafinga mjini mh. Cosato Chumi.

Sauti ya Cosato Chumi

Mkurugenzi wa teknolojia ya nishati jadidifu na mbadala, Advera Mwijage kwa niaba ya mkurugenzi wa wakala wa nishati vijijni REA, amesema wanalojukumu la kuhakikisha jamii inapata uwelewa wa matumizi ya nishati safi ya kupikia na kusifu mwamko wa wanawake katika kutimiza azma ya serikali.

Sauti ya Advera Mwijage

Vilevile Mwijage ameagiza kampuni zote zinazosambaza gesi kuhakikisha wanasambaza kwenye maeneo ya vijijni ili kupunguza gharama za kuifuata maeneo ya mijini jambo linaloweza kukwamisha Maendeleo.
Baadhi ya wanufaika wa mitungi hiyo ya nishati ya gesi, wameishukuru serikali pamoja na mbunge kwani imerahisisha majukumu na kunusuru afya za watanzania huku wakiomba kutazamwa kwa jicho la kipekee gharama za nishati hiyo.

Sauti ya wanufaika mitungi ya gesi

Mipango ya serikali ni kusambaza mitungi ya gesi 452,400 pamoja na kuboresha upatikanaji wa nishati safi na salama ya kupikia asilimia 75 ifikapo mwaka 20230 Hadi sasa mitungi 74,600 imesambazwa vijijni.