Mufindi FM

TADIO yawanoa wanahabari Mufindi FM

27 September 2023, 20:07

Waandishi wa habari Mufindi FM wakiwa katika mafunzo ya urushaji maudhui mtandao kupitia radio.Picha na Kelvin Mickdady

Na Isaya Kigodi -Mufindi

Mtandao Wa Radio Jamii nchini( TADIO) umetoa mafunzo ya Ndani kwa waandishi Wa habari Wa kituo Cha jamii Mufindi FM.

Mafunzo hayo ya siku Moja yametolewa Leo September 27,2023 na Mkufunzi Amua Rushita kutoka mtandao Wa TADIO kwa lengo la kuwaimarisha waandishi Wa habari kwenye matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii kwenye usambazaji wa habari.

Waandishi hao wamesisitizwa pia kuendana na kasi ya matumizi ya mitandao ya kijamii kusambaza taarifa ambazo zinawagusa wananchi wa ngazi ya chini kwenye jamii.

“Tutumie ukurasa huu Wa radio TADIO kuandika taarifa zinazoizunguka jamii yetu, ili kuisaidia kutatua changamoto zinazoikabili ” Amesisitiza Amua Rushita mkufunzi kutoka TADIO.

Nao waandishi wa habari wamemshukuru mkufunzi Amua Rushita kwa muda wake aliyoutenga kwaajili ya kutoa mafunzo na kuahidi kushirikana ili jamii iweze kufikiwa na habari ambazo zinakuwa zimeandaliwa na kituo.

Kituo Cha radio MUFINDI FM kinamilikiwa na halmashauri ya Wilaya ya Mufindi na kinajikita kutoa habari za ndani ya Wilaya na nje ya Wilaya.