Mufindi FM
Mufindi FM
22 July 2026, 10:35 am

Mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini Mhe. Dickson Lutevele Villa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ugute kilichopo katika kaya ya Isalavanu ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kata kwa kata, kijiji kwa kijiji ndani ya jimbo hilo. Picha na Marko Msafiri.
Na Marko Msafiri
Serikali imetangaza bei elekezi ya mbolea ya ruzuku kwa mwaka wa fedha 2026/2027, huku ikielezwa kuwa, kuna ongezeko ikilinganishwa na mwaka uliopita, linalotokana na gharama za uzalishaji na usafirishaji.
Akizungumza katika ziara ya Mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini, iliyofanyika katika kata ya Isalavanu, Afisa Kilimo wa Mji Mafinga, ndg. Baraka Mwamanga, ametaja bei hizo elekezi ambapo amesema, DAP inauzwa kwa Tshs 89,000/=, Urea Tsh 84,000/= na CAN inauzwa kwa Tshs 66,000/=.
Aidha Mwamanga, amesema pembejeo za ruzuku zitapatikana katika kipindi chote cha msimu wa kilimo, licha ya changamoto za upatikanaji zilizojitokeza katika miezi michache iliyopita.
Sauti Afisa Kuliko Bw. Mwamanga.
Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Mafinga Mjini, Mhe. Dickson Lutevele Villa, amemtaka Afisa Kilimo kuhakikisha anapatikana wakala wa pembejeo za kilimo katika Kata hiyo ili kupunguza usumbufu wa wananchi kulazimika kufuata huduma hizo mjini Mafinga.
Sauti Mhe. Villa.

mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini Mhe Dickson Lutevele Villa akizungumza na wananchi wa kijiji cha kikombo kilichopo katika kata hiyo ya Isalavanu, wakati wa ziara yake katani humo. Picha na Marko Msafiri.
Nao baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano huo akiwemo Meshaki Kakingo, wameiomba serikali kuongeza kiwango cha ruzuku kwenye mbolea ili kupunguza gharama kwa wakulima na kuwawezesha kuendelea kuzalisha kwa tija.
Sauti mwananchi.
Katika hatua nyingine, wananchi wa kata hiyo ya Isalavanu, wamempongeza Mhe. Villa kwa ushirikiano wake na jamii, wakisema amekuwa msikivu wa kero zao na mstari wa mbele katika kusukuma maendeleo ya kata hiyo.
Sauti Wananchi pongezi.

Pichani ni wananchi wa kijiji cha Ugute wakimsikiliza Mbunge wa jimbo la Mafinga mjini Mhe. Dickson Lutevele Villa wakati wa ziara yake ya kata kwa kata, kijiji kwa kijiji aliyoifanya hivi karibuni. Picha na Marko Msafiri.