Mufindi FM

Sekta ya Maendeleo Mufindi yapewa kongole

12 September 2023, 11:55

Lengo letu ni kusaidia sekta zote kama tulivyoanza na sekta ya Afya na shughuli mbalimbali za maendeleo

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mufindi Festo Mgina akipokea Cheti cha Pongezi kutoka kwa mkuu wa taasisi ya Vijana ( Youth Agency Mufindi) Geoff Fox, Picha Kelvin Ayub

Na Kelvin Ayub

Familia ya Geoff fox imekabidhiwa hati ya pongezi kama utambuzi wa mchango wao katika sekta ya maendeleo ya jamii wilayani mufindi.

Hafla hiyo fupi ya pongezi  imefanyika kata ya luhunga Kijiji cha igoda wilaya ya mufindi ikiwa ni sehemu ya shukrani kwa kuendelea kutekeleza miradi  ya ujenzi wa barabara,ujenzi wa shule ,ujenzi wa uchimbaji wa visima vya maji na utoaji elimu ya ujasiliamali kwa vijana.

Aidha familia ya mzee Geoff fox Pamoja na taasisi yake ya Vijana ( Youth Agency Mufindi) imekabidhi  majengo mawili ya zahanati ya igoda na  nyumba moja ya mganga mfawidhi   huku wakiendelea kutekeleza miradi ya maendeleo ya jamii  ikiwemo  uwezeshaji wa wanawake kiuchumi,uwezeshaji wa vijana  kielimu.

Sauti ya Nicko Fox msemaji wa Taasisi yake ya Vijana ( Youth Agency Mufindi)

Kwa upande wa Mwenyerkiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi mh. Festo Mgina ameushukuru Uongozi wa Familia hiyo na kutoa rai kwa wananchi kulinda na kutunza miradi ili wadau wa maendeleo ya jamii waendelee kuleta fursa.

Ikumbukwe mradi huo wa ujenzi wa zahanati ya igoda umegharimu kiasi cha shilingi Millioni 300  pamoja na vifaa tiba ambapo familia na taasisi yake (youth agency mufindi),   Geoff Fox Imeweza kuzitumia kukamilisha mradi huo na kuukabidhi kwa halmashauri ya Mufindi.