Mufindi FM

Wamiliki viwanda Mufindi watakiwa kusimamia maslahi ya wafanyakazi

10 October 2023, 19:16

Na Kefa Sika/Mafinga

Mkuu wa wilaya ya Mufindi Dkt. Linda Salekwa amewataka wamiliki na wasimamizi wa viwanda wilayani Mufindi kusimamia taratibu na sheria za ufanyaji kazi ili kuwasaidia wananchi.

Salekwa ameyasema hayo katika ziara ya viwandani mjini Mafinga kuwa kila msimamizi na mmiliki wa kiwanda ahakikishe kuna mazingira rafiki ya kufanya kazi ikiwemo kuwalipa ujira kwa wakati.

Sauti ya DC Linda Salekwa

Sanjari na hayo Salekwa amesema kuwa wamiliki wenye viwanda na makampuni wanatakiwa kulipa madeni kabla ya kuchukuliwa sheria za kinidhamu na serikali.

Sauti ya DC Linda Salekwa

Awali baadhi ya wasimamizi wa viwanda mjini Mafinga wamesema kuwa changamoto kubwa inayowakabili ni ubovu wa miundombinu hivyo kuchelewa kufanya kazi.

Sauti ya wasimamizi viwanda

Mkuu wa wilaya na kamati ya usalama wamefanya ziara kwenye viwanda mjini Mafinga ikiwemo kiwanda cha BEST kinachojihusisha kutengeneza mkaa wa kisasa, kiwanda cha Shedafa na Qwihaya vinavyojihusisha na utengenezaji wa nguzo za umeme.