Mufindi FM

Migogoro ya ndoa si kuchana vyeti

12 May 2026, 8:35 pm

Pichani ni msaidizi wa masuala ya kisheria kutoka shirika la Legal Right Enlightment Organisation, Jimmy Mgovano akiwa katika mahojiano maalumu na kituo cha redio cha Mufindi Fm.Picha na Mwanaidi Ngatala.

Ndoa ni muungano wa hiari wa kisheria, kijamii, na mara nyingi kiroho, kati ya mwanamke na mwanamume (au watu wawili kulingana na sheria husika) kuishi pamoja kama mume na mke. Ni mkataba unaotambuliwa rasmi unaoweka haki, wajibu, ushirikiano, na urithi kati ya wanandoa na familia.

Na Wityness Alex

Wanandoa wameshauriwa kuacha tabia ya kuharibu cheti cha ndoa kwa makusudi pindi inapotokea wamehitilafiana ili kuharibu mchakato wa madai ya talaka kwani kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.

Kwa mujibu wa sheria ya ndoa ya Tanzania ya mwaka 1971, ndoa ni hiari baina ya watu wawili hivyo wanandoa wanatakiwa kuwa makini katika maamuzi hayo kabla kuingia viapo rasmi vya ndoa.

Msaidizi wa masuala ya kisheria kutoka shirika la Legal Rihgt Enlightment Organisation, Jimmy Mgovano ametanabaisha kwamba cheti cha ndoa ni nyaraka ya serikali hivyo atakayebainika kukiharibu kwa makusudi atakumbana na mkono wa sheria.

Sauti Jimmy shitaka

Kadhalika Bw.Mgovano hapa anaeleza utaratibu wa kupata cheti cha ndoa endapo kimepotea au kuharibika kwa bahati mbaya.

Sauti Jimmy cheti

Sanjari na hayo Bw. Mgovano amewashauri wanandoa kutunza cheti cha ndoa mara baada ya ndoa kukamilika ili kuepuka usumbufu wakati wa ufuatiliaji wa mirathi pindi mwenzi mmoja anapofariki au wakati wa talaka pindi ndoa hiyo itakapohitajika kutenganishwa.

Sauti Jimmy wito

Pichani ni kibonzo kikionyesha umuhimu wa cheti cha ndoa kwa wanandoa. Picha kutoka maktaba ya RITA.

Hivi karibuni huko nchini Nigeria wanandoa waliibua gumzo na mjadala mkali mitandaoni baada ya kuchana vyeti vyao vya ndoa wakati wa sherehe ya harusi yao kwa madai kuwa ni ishara ya kiapo cha kujitolea wakiamini kuwa kutokuwepo kwa hati hiyo hakuna uwezekano wa talaka ya kisheria na hivyo wataishi pamoja kwa amani mpaka kifo kiwatenganishe.