Mufindi FM

Mbunge Chumi akabidhi ambulance Ifingo

21 March 2024, 18:33

Viongozi na wananchi wa kata ya kinyanambo halmashauri ya mji Mafinga wakiwa katika shamlashamla za kupokea gari la wagonjwa kwenye kituo Cha afya Ifingo leo machi 21 2024. Picha na Hussein Nyalusi.

Na Bestina Nyangaro/Mafinga

Mbunge wa Jimbo la Mafinga mjini Mh. Cosato David Chumi amekabidhi gari la kubebea wagonjwa (ambulance) katika kituo cha afya Ifingo kata ya Kinyanambo.

Hafla ya kukabidhi gari hilo imefanyika leo machi 21 2024, kwa lengo la kurahisisha usafiri kwa wagonjwa, akisema hata hivyo juhudi za wananchi zimehusika kuhakikisha mradi unakamilika kikamilifu.

Sauti ya Cosato Chumi

Katika hatua nyingine Mh.Chumi ameahidi shilingi million 7 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za mtaa wa Mizani na mtaa wa Gangilonga.

Diwani wa kata ya Kinyanambo ambaye pia ni mwenyekiti wa halmashauri ya mji Mafinga Mh. Reginald Kivinge amekiri kuwa jitihada za mbunge ni za vitendo ambazo zitaokoa maisha ya wananchi.

Sauti ya Reginald Kivinge

Awali mganga mkuu wa halmashauri ya mji Mafinga Dkt. Chitopela Bonavanture amesema pamoja na kuwepo kwa usafiri huo, hivi karibuni huduma za upasuaji kwa wajawazito zitaanza kutolewa kituoni hapo kupunguza umbali na msongamano uliokuwa ukiwakabili kwenye hospitali ya mji Mafinga.

Sauti ya Chitopela Bonavanture

Ujenzi wa kituo cha afya Ifingo ulianza mwaka 2021 na kukamilika mwaka 2023 kwa sasa tayari huduma zinatolewa kwa wananchi.