Mufindi FM

Mkali Wa ‘Draft’ Mufindi Asakwa

12 September 2023, 06:41

Baadhi ya washiriki wakichuana kumpata mshindi wa mchezo wa bao, katika uwanja wa mashujaa uliyo Mafinga mjini. Picha na Kelvin Mickdady

Na Kelvin Mickdady -Mafinga.

Mashindano ya Bao (Draft) Mufindi Yamefunguliwa Hii Leo katika Uwanja wa Mashujaa kwa hatua za makundi sita kupangwa na kuanza kupimana ufahamu kwa kusukuma Kete.

Aidha mratibu wa Mashindano hayo Hussein Tulka amesema kuwa huu ni mwanzo tu kwani wanatarajia kufanya Mashindano mengi makubwa huku akitoa shukrani za dhati kwa mdhamini mkuu wa Mashindano hayo Katibu Itikadi na uenezi Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mufindi Ndg.Dickson Lutevele (Villa) kwa kuonyesha moyo wa Umoja kwa Vijana.

Hata hivyo Mechi kadhaa za Hatua za Makundi Yamefanyika Leo ambapo kila Kundi limetoa Watu Wawili ambao watacheza katika Hatua ya Kumi na sita Bora, Huku nusu Robo fainali, Nusu Fainali, na Fainali kuchezwa Kesho.

Ikumbukwe Zawadi kwa Mshindi wa kwanza ni Pesa taslimu za Kitanzania Shilingi Laki tatu (300,000), Mshindi wa Pili atajinyakulia Shilingi Laki mbili (200,000) Na Mshindi wa tatu atapata Shilingi Laki Moja (100,000).