Mufindi FM

Wakulima Mufindi kunufaika na kipima udongo

21 September 2023, 17:19

Wataalam kutoka shirika la Care na WWF Alliance pamoja na wakulima wilayani Mufindi wakiwa katika moja ya shamba darasa. Picha na Care.

Na Jumanne Bulali

Kifaa cha kupimia udongo kinatarajiwa kuwa na tija kwa wakulima wengi wilayani Mufindi kwani wataweza kupanda mazao kulingana na aina ya ukanda wao.
Kifaa hicho kilikabidhiwa mapema mwezi huu na katibu tawala wilaya ya Mufindi ndg. Frank Sichalwe na kuwataka maafisa ugani kutoa huduma hiyo pasipo kumtoza chochote mkulima.
Katika mahojiano maalum na afisa pembejeo halmashauri ya wilaya ya Mufindi Ndg. Vasco Ngimbuchi amesema kwamba, halmashauri hiyo imepanga kuchukua kila aina ya udongo katika kata zote na kuwashauri wakulima walime aina ipi ya mazao.

Sauti ya Afisa pembejeo Vasco Ngimbuchi

Naye Meneja Shirika la Care WWF Alliance Dkt. Abubakary Kijoji ambalo linajihusisha na masuala ya kilimo hasa shamba darasa amesema wamekuwa wakiwasaidia wakulima kulima mazao kutokana na eneo walilopo.

Sauti ya Abubakary Kijoji

Sambamba na hayo Dkt. Kijoji ameongeza kuwa katika kutoa elimu kwa wakulima huwa wanawaonesha wakulima aina mbalimbali za mbegu ili kumpa mkulima machaguo tofauti.

Sauti ya Kijoji

Ili Mkulima aweze kunufaika na kilimo chake wataalam wanashauri ni vyema akazingatia matumizi ya mbegu kutokana na aina ya udongo, kupalilia kwa wakati na kutumia mbolea.