Mufindi FM

Ni Muungano wa usafi

19 April 2024, 20:04

Viongozi mbalimbali wilayani Mufindi Wakishiriki zoezi la Usafi wa mazingira kijiji cha Nzivi.Picha na Jackson Machowa.

Na Jackson Machowa-Mufindi

Kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano Tanganyika na Zanzibar yatakayoadhimishwa April 26 wakurugenzi wa halmashauri za Mji wa Mafinga na Wilaya ya Mufindi wamewaongoza watumishi wa halmashauri hizo kufanya usafi katika hospitali ya wilaya ya Mufindi iliyoko katika kijiji cha Nzivi.
Wakizungumza mara baada ya kumalizika kwa shughuli za usafi, Mkurugenzi Bwana Mashaka Mfaume kutoka halmashauri ya wilaya ya Mufindi na Bi Federica Myovela mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mji wa mafinga wamesema zoezi hilo litakuwa endelevu ili kuimarisha usafi wa mazingira wilayani hapa.

Sauti ya DED Mfaume, Bi Fedelica

Akimwakilisha mkuu wa wilaya ya Mufindi Dkt Linda Salekwa katika shughuli hiyo, Afisa Tawala Bwana Robart Kilewo amesema maadhimisho ya muungano kwa mwaka huu yatahusisha kufanyika kwa shughuli za kijamii zaidi ili kuikumbusha jamii kuhusu dhima na umuhimu wa uwepo wa muungano.
Aidha Bwana Kilewo amewataka wakurugenzi watendaji wa halmashauri zote mbili za mji wa Mafinga na wilaya ya Mufindi kuepuka matumizi makubwa ya fedha za serikali katika kuratibu na kufanikisha shughuli za matukio yote ya kuazimisha sherehe za muungano.

Sauti ya Kilewo

Jamuhuri ya watu wa Tanganyika waliokuwa chini ya utawala wa Mwl. Julius Nyerere waliungana na Jamuhuri ya watu wa Zanzibar waliokuwa chini ya utawala wa Abeid Karume mwaka 1964 na kuzalisha Taifa moja la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania huku Kauli mbiu za sherehe hizo kwa mwaka huu 2024 ni Tumeshikamana, Tumeimarika, Kwa maendeleo ya Taifa letu.