Mufindi FM

Kushika simu ya mpenzi wako ni kosa kisheria

15 September 2023, 12:36

Kupekua simu ya mwenza au mpenzi imetajwa kuwa sababu ya mahusiano mengi kuvunjika bila kujua kama ni kosa kwa mujibu wa sheria.

Na John Selijo – Mufindi l FM

Wanaondoa na wapenzi wameshauriwa kuacha kupekua na kukagua simu za wenza wao kwani kufanya hivo nikosa kisheria.
Akizungumza na Mufindi Fm Msaidizi wa kisheria kutoka Shirika la Legal Right Enlargment Organization lililopo Mjini Mafinga Jimmy Mgovano kwamba nikosa kisheria kuingilia faragha ya mtu bila ruhusa.

Sauti ya Mwanasheria Mgovano

Naye Msaikolojia Cancellor Dkt. Briano Richman ameeleza kuwa kuna baadhi ya athari zinazoweza kumpata mtu anayekagua simu ya mwenza wake, ikiwemo presha pamoja na kuongeza migogoro katika ndoa zao.

Sauti ya Dkt Richman

Sanjari na hayo Dkt. amewataka wananchi kuachana na tabia ya kupekua simu za wenza wao ili kuweza kudumisha ndoa zao.

Sauti ya Dkt.Richman