Mufindi FM

Waziri Mkuu akemea unyang’anyi, kero ya barabara ikitawala

4 May 2026, 8:07 pm

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba akizungumza na wananchi sambamba na kusikiliza kero zao katika viwanja vya shule ya msingi Igowole, wakati wa ziara yake ya kikazi wilayani Mufindi mkoani Iringa. Picha na Marko Msafiri.

Kwenye vyanzo vyangu nimeambiwa upo utaratibu na wengine ni wa serikali, wengine ni wa sekta binafsi, vijana wetu wanafanya kazi na malipo yao hawapewi, ila magari wanabadilisha kila siku, lakini hela za kuwalipa wanyonge hawana “Dkt. Mwigulu

Na Marko Msafiri

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema serikali haitavumilia vitendo vya ukiukwaji wa haki za wananchi, akisisitiza kuwa yeyote anayewanyima wananchi haki zao za msingi atachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa sheria.

Akizungumza katika ziara yake ya kikazi wilayani Mufindi, mkoani Iringa, Dkt. Nchemba amesema serikali imejipanga kuhakikisha wananchi wanapata haki na huduma stahiki bila vikwazo.

Sauti Dkt. Mwigulu Unyang’anyi

Wananchi wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali katika ziara ya Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba wilayani Mufindi. Picha na Christoggon Ngoloki.

Katika hatua nyingine, Dkt Mwigulu ameagiza kuanza kwa ujenzi wa barabara ya Mafinga-Mgololo, barabara ya Nyololo-Mtwango pamoja na mwendelezo wa sehemu iliyobaki katika barabara ya Mtili-Ifwagi-Lulanda, akisisitiza ahadi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan zinapaswa kutekelezwa bila kuchelewa.

Sauti Dkt. Mwigulu barabara.

Wabunge wa mkoa wa Iringa, wakiongozwa na Mbunge wa jimbo la Mufindi Kusini, David Kihenzile, wameiomba Serikali “kuvunja mfupa huo mgumu” kwa kuanza ujenzi wa miradi hiyo, wakieleza kuwa kukamilika kwake kutafungua fursa mbalimbali za kiuchumi na kuharakisha maendeleo ya wilaya ya Mufindi.

Sauti Wabunge.