Mufindi FM
Mufindi FM
28 April 2026, 11:05 am

Pichani ni Fadhil Elisha Mtega na David Michael Lugendo wakazi wa Usokami, wilaya ya Mufindi waliohukumiwa miaka miwili ( Kila mmoja) na Mahakama ya Hakimu mkazi ya wilaya hiyo. Picha na Witness Alex.
Kwa mara ya kwanza duniani suala hilo liliripotiwa kusini mashariki kwa bara la Asia ambapo walilipa jina la “Koro Syndrome” wakihusianisha na mnyama kobe ambaye anaweza kuficha kichwa chake na kukitoa kulingana na wakati fulani, pia Bara la Ulaya na Mwaka 2023 ikaripotiwa Afrika na ni Kusini Mashariki kwa Nigeria.
Na Witness Alex
Mahakama ya hakimu mkazi wilaya Mufindi imewahukumu miaka miwili jela kila mmoja Fadhili Elisha Mtega (26), Mfipa, Mkazi Wa Usokami, Na David Michael Lugendo, Miaka 28, Muha, Mkazi Wa Usokami kwa kosa la kumshambulia Raymond Shoma Lighali,Miaka 26, Daktari Usokami, Msukuma, Mkazi Wa Usokami.
Hukumu hiyo imetolewa leo na hakimu mkazi wa wilaya ya Mufindi Mhe.Sekela Kyungu ambapo imeelezwa kuwa Watuhumiwa hao April 06, 2026 majira ya saa moja jioni katika Kijiji cha Usokami, Walimshambulia Daktari huyo maeneno mbalimbali ya mwili ikiwemo Kichwani, Usoni, jicho la kulia na sehemu mbalimbali za mwili.
Imeelezwa chanzo cha Daktari huyo kushambuliwa ni Baada Ya Fadhil Elisha Mtega, Kudai Sehemu Zake Za Siri Hazionekani mbinu aliyoitumia kuzua taharuki na kuanza kumshambulia Kwa Mbao, Stuli Za Kukalia Na Ngumi.
Watuhumiwa hao wamehukumiwa kwa kosa la kujeruhi vibaya kinyume na kifungu cha 225 cha Sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16, marejeo ya 2023.
Katika shauri lingine Mnamo Tarehe 07/04/2026 Majira Saa 1:00 mchana Polisi Mafinga, Kata Ya Boma, Tarafa Ya Ifwagi, Wilaya Ya Mufindi Na Mkoa Iringa Mussa Kaundi, (39), Mpogolo, Machinga akiwa Mtaa wa Pipeline, alitoa Taarifa Za Uongo Na Kuzua Taharuki Kituo Cha Mafuta Kiitwacho Ngoli Mafinga Kuwa Nyeti Zake Zimetoweka Baada Ya Kuguswa Bega.
Inadaiwa kuwa siku hiyo Mtu anayefahamika kwa jina la Androis Kudzai Kufakwepasi, (31) raia wa Zimbabwe, Alihitaji Kununua Saa Ya Mkononi, Lakini Hawakuelewana Bei Ndipo Mhanga Akamrudishia Saa Hiyo Na Kuondoka Ndipo Mtuhumiwa Alianza Kupiga Kelele Kuwa Nyeti Zake Zimetoweka Kwa Kuwaambia Bodaboda Wanaojaza Mafuta Sheli Ya Ngoli Hali Hiyo Ilipelekea Kuzua Taharuki Na Baadhi Kutaka Kumshambulia Mhanga.
Shauri hilo bado linaendelea Mahakama Ya Mwanzo Chini ya Hakimu mkazi mahakama ya mwanzo Mhe.Maria Bahati Sumay.