Mufindi FM
Mufindi FM
15 October 2026, 1:24 pm

Makamu wa Rais kutembelea mradi wa umeme wa TAZA wilayani Mufindi Oktoba 17, 2026 ili kujionea maendeleo ya mradi huo wa kimkakati.
Na Jumanne Bulali
Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Mheshimiwa Dkt. Linda Salekwa, ametangaza ujio wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, wilayani humo, unaotarajiwa kufanyika Oktoba 17, 2026.
Akizungumza na Mufindi FM Radio, Dkt. Salekwa amesema kuwa wakati wa ziara hiyo, Makamu wa Rais atatembelea mradi mkubwa wa umeme wa TAZA unaounganisha Tanzania na Zambia.
Aidha, Dkt. Salekwa amesema kuwa uwepo wa mradi huo Wilayani Mufindi unatarajiwa kuchangia kuboresha upatikanaji wa nishati ya umeme wa uhakika kwa matumizi ya wananchi na viwandani na kuchochea shughuli za ukuaji wa uchumi wilayani humo.
Mradi huo wenye thamani ya shilingi bilioni 69 unatekelezwa katika Kijiji cha Kisada, Kata ya Bumilahinga, Wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa.
Ziara hiyo inatarajiwa kutoa fursa ya kufahamu maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo wa kimkakati wa kuunganisha mifumo ya umeme kati ya Tanzania na Zambia.