Mufindi FM

Mufindi yaandaa Jukwaa la Uwekezaji Kutangaza Fursa za Kilimo, Ufugaji na Biashara

7 October 2026, 9:24 pm

Mkuu wa wilaya ya Mufindi Mh. Dkt Linda Salekwa akizungumzia fursa za uwekezaji katika mahojiano maalumu na redio Mufindi FM. Picha na Christogon Ngoloki.

Kufanyika kwa Jukwaa hilo la maonesho ya fursa za uwekezaji kunatajwa kuwa nguzo muhimu katika kuchochea na kuinua uchumi wa wilaya ya Mufindi na Taifa kwa ujumla

Na Jackson Machowa.

Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa imeanzisha Jukwaa la Uwekezaji na Maonyesho ya Fursa za Uwekezaji ikiwa na lengo la kutangaza fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo wilayani humo na kuwaunganisha wawekezaji na sekta zenye uwezo wa kuchochea ukuaji wa uchumi.

Akizungumza wakati wa mahojiano na Mufindi FM kupitia kipindi cha Morning Gia, Dkt. Salekwa amesema wilaya ya Mufindi ina fursa mbalimbali katika sekta za kilimo, ufugaji, uvuvi na biashara ambazo zinahitaji kutangazwa zaidi ili kuwafikia wawekezaji kutoka ndani na nje ya wilaya.

Sauti ya mkuu wa wilaya Mufindi Mh. Dkt Linda Salekwa

Amesema kupitia Mufindi Investment Forum and Expo, wilaya inalenga kuwaunganisha wawekezaji na fursa zilizopo, huku ikihamasisha wafanyabiashara na wawekezaji kuzitumia fursa hizo kwa ajili ya kuongeza uzalishaji, ajira na kuchochea maendeleo ya kiuchumi.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Mufindi Mh. Dkt Salekwa

Aidha Mh. Dkt Salekwa ameongeza kuwa maonyesho hayo ambayo yatazinduliwa rasmi na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, yatafanyika kwa muda wa siku tano kuanzia Oktoba 16 hadi 20, 2026.

Mkuu wa wilaya ya Mufindi Mh. Dkt Linda Salekwa akizungumzia fursa za uwekezaji katika mahojiano maalumu na redio Mufindi FM. Picha na Christogon Ngoloki.

Ameongeza kuwa mpango huo pia unalenga kuhakikisha wawekezaji wanaofuata sheria na taratibu wanapata mazingira yanayowawezesha kufanya shughuli zao kwa ufanisi na kuchangia maendeleo ya wilaya.