Mufindi FM
Mufindi FM
19 October 2026, 1:55 pm

Wilaya ya Mufindi inasifika kwa ardhi yenye rutuba inayofaa kwa kilimo cha mazao mbalimbali, hali inayoifanya kuwa eneo lenye fursa nyingi za uwekezaji zinazoweza kuchochea ukuaji wa uchumi wa wananchi na Taifa kwa ujumla
Na Jumanne Bulali
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Dkt. Pius Chaya, amesema Wilaya ya Mufindi ni miongoni mwa maeneo ya kimkakati katika kufanikisha utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2050, akiwataka wawekezaji na wafanyabiashara kutumia fursa zilizopo kuchochea ukuaji wa uchumi.
Dkt. Chaya ameyasema hayo, alipomwakilisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, katika ufunguzi wa Maonesho ya Mufindi Investment Forum and Expo 2026, yanayofanyika Mafinga Mjini, mkoani Iringa…..maonesho 01….

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Dkt. Linda Salekwa, amesema maonesho hayo yanaunga mkono utekelezaji wa Dira ya Taifa kwa kutangaza fursa za uwekezaji na kuhamasisha maendeleo endelevu. Naye Mbunge wa Vijana kutoka Iringa, Jasmine Ng’umbi, amewataka vijana kutumia maonesho hayo kujipatia fursa za kiuchumi na kuongeza kipato….maonesho 02….
Maonesho hayo yenye kaulimbiu ya “Connect, Invest and Grow” (Unganisha, Wekeza na Kua Kiuchumi), ni ya siku tano kuanzia Oktoba 16 hadi 20, 2026.