Mufindi FM

DC Mufindi aweka mambo wazi kuhusu eneo la ujenzi wa shule Nandala

9 November 2026, 11:28 am

Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Dkt. Linda Salekwa, akizungumza na baadhi ya wananchi pamoja na viongozi wa Serikali ya Kijiji cha Nandala.

DC Mufindi, Dkt. Linda Salekwa, aeleza msimamo kuhusu eneo la ujenzi wa shule ya sekondari Kijiji cha Nandala, Kata ya Ihanu.

Na Jumanne Bulali

Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Mheshimiwa Dkt. Linda Salekwa, ametatua mgogoro wa ardhi uliokuwa ukihusu ombi la mwekezaji wa taasisi ya Village School Tanzania kupewa eneo kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari katika Kijiji cha Nandala, Kata ya Ihanu, Wilayani Mufindi.

Dkt. Salekwa amefikia uamuzi huo wakati wa ziara yake katika kijiji hicho, ambapo baadhi ya wananchi walieleza nia yao ya kutaka eneo hilo litolewe kwa mwekezaji huyo ili aweze kujenga shule ya sekondari.

Sauti ya DC Dkt Linda Salekwa

Hata hivyo, Mkuu huyo wa Wilaya aliwaeleza wananchi kuwa eneo hilo tayari limeingizwa katika Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi na kubainisha kuwa mkataba uliokusudiwa kuingiwa kati ya kijiji na mwekezaji huyo haukuwa umeweka bayana masharti na maslahi ya pande zote.

Sauti ya DC Dkt Linda Salekwa

Awali, Afisa Ardhi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, Ally Shelukindo, alieleza kuwa Kijiji cha Nandala kiliingizwa katika Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi tangu mwaka 2020.

Sauti ya Ally Shelukindo

Katika hatua nyingine, Dkt. Salekwa amewataka wananchi kuwa makini na kutafakari kwa kina kabla ya kufanya maamuzi yanayohusu matumizi na usimamizi wa rasilimali za jamii, ikiwemo ardhi, ili kuepuka migogoro inayoweza kujitokeza baadaye.