Mufindi FM

Mtoto wa miaka 13 afariki dunia Mafinga, madai ya kujinyonga yafuatiliwa

22 October 2026, 8:39 pm

Picha ya mfano wa kamba inayohusishwa na vitendo vya kujidhuru. Picha: Mtandao.

Taarifa za awali kuhusu kifo cha mtoto Judith Mwenzegula, mwenye umri wa miaka 13, mkazi wa Mafinga mkoani Iringa, huku mazingira ya tukio hilo yakisubiri uthibitisho rasmi kutoka kwa mamlaka husika.

Na Sofia Moses

Mtoto Judith Mwenzegula, mwenye umri wa miaka 13, mkazi wa Mtaa wa Mji Mwema, Halmashauri ya Mji Mafinga, Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa, amefariki dunia katika mazingira ambayo bado hayajathibitishwa rasmi.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na viongozi wa eneo hilo na wanafamilia, tukio hilo linadaiwa kutokea Oktoba 21, 2026, majira ya saa sita mchana, baada ya mtoto huyo kuhojiwa na mama yake wa kambo kuhusu upotevu wa Shilingi 2,000 zilizotokana na mauzo ya mikate.

Taarifa za awali zinaeleza kuwa mtoto huyo anadaiwa kufariki baada ya kujinyonga kwa kutumia kitenge kwenye mti uliokuwa karibu na nyumbani kwao,Hata hivyo, mazingira na chanzo cha kifo hicho bado havijathibitishwa rasmi na mamlaka husika.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Mji Mwema, Castory Nditu, amesema hakuwa amepokea taarifa zozote kuhusu migogoro au vitendo vya ukatili ndani ya familia ya mtoto huyo kabla ya tukio hilo.

Sauti ya mwenyekiti wa mtaa wa mji mwema Castory Nditu

Nditu ametoa wito kwa wazazi na walezi kuimarisha malezi na mawasiliano na watoto, ili kuwasaidia kukabiliana na changamoto zinazoweza kujitokeza katika maisha yao.

Sauti ya mwenyekiti wa mtaa wa mji mwema Castory Nditu

Kwa upande wao, mama mlezi wa marehemu, Yasinta Msigwa, pamoja na Edina Msigwa, wamesema wameshtushwa na tukio hilo, wakieleza kuwa mtoto huyo alikuwa akiishi nao katika mazingira ya upendo na malezi mema.

Sauti ya mama mlezi wa marehemu Yasinta Msigwa pamoja na mama mdogo mlezi wa marehemu Edina Msigwa

Redio Mufindi FM inaendelea kufuatilia taarifa rasmi kutoka kwa Jeshi la Polisi kuhusu tukio hilo.